عَنْ أَبِي مَالِكٍ الْأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ للهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ للهِ تَمْلَآنِ - أَوْ تَمْلَأُ - مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا»

Kutoka kwa Abu Malik Al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu awe radhi naye ambaye amesema:

Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: 1- “Usafi ni nusu ya imani, 2- Na kusema: Alhamdulilaah (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) inajaza mizani. 3- Na kusema: Subhaanallah) Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, hujaza au huyajaza yaliyo baina ya mbingu na ardhi. 4- Sala ni Nuru. 5- Na sadaka ni Ushahidi( juu ya Imani). 6- Subira ni mwangaza. 7- Na Qur’ani ni hoja kwako au dhidi yako. 8- Watu wote huondoka asubuhi, kwa hivyo yupo anayeiuza nafsi yake na akaiacha huru na mwengine akaiangamiza.”


Al-Harith bin Al-Harith

Al-Harith bin Al-Harith, na ikasemwa jina lingine tofauti na hilo, Abu Malik, Al-Ash’ari, Al-Shami, aliyesilimu na akafuatana na Mtume rehma na amani zimshukie na akapigana pamoja na Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, amesema Mtume kuhusu yeye: “Ewe Mola, mrehemu Ubaid Abi Malik Al-Ash’ari, na umjaalie awe juu ya watu wengi.” [1]  alifariki dunia kwa tauni mwaka. (18 AH) [2]

Marejeo

1. Imepokewa na Ahmad (22907).

2. Tazama ufafanuzi wake  katika: “Al-Isti’ab fi Ma’rifat al-Ashab” na Ibn Abd al-Barr (1/ 284), “Historia ya Damascus” cha Ibn Asaker (67/ 187), “Asad al- -Ghaba” cha Ibn al-Athir (5/ 272).


Miradi ya Hadithi