عَنْ أَبِي مَالِكٍ الْأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ للهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ للهِ تَمْلَآنِ - أَوْ تَمْلَأُ - مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا»

Kutoka kwa Abu Malik Al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu awe radhi naye ambaye amesema:

Mtume rehma na Amani zimshukie amesema: 1- “Usafi ni nusu ya imani, 2- Na kusema: Alhamdulilaah (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) inajaza mizani. 3- Na kusema: Subhaanallah) Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, hujaza au huyajaza yaliyo baina ya mbingu na ardhi. 4- Sala ni Nuru. 5- Na sadaka ni Ushahidi( juu ya Imani). 6- Subira ni mwangaza. 7- Na Qur’ani ni hoja kwako au dhidi yako. 8- Watu wote huondoka asubuhi, kwa hivyo yupo anayeiuza nafsi yake na akaiacha huru na mwengine akaiangamiza.”


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi mtukufu:

“Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha”

[Al-Baqara: 222]

Na akasema Allah Mtukufu:

. “Na Siku hiyo kipimo kitakuwa kwa Haki. Basi watakao kuwa na uzani mzito, hao ndio watakao fanikiwa (8) Na watakao kuwa na uzani khafifu, basi hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzipinga Ishara zetu”

[Al-A’raf: 8, 9]

Mwenyezi Mungu amesema:

. “Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo” .

[Al-Tawba: 111]

Akasema pia:

“Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu”

[Al-Ankabut: 45].

Akasema pia:

“Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu”

[Al-Zumar: 10].

Miradi ya Hadithi