عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ«مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهَا أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ» يَعْنِي أَيَّامَ الْعَشْرِ، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟ قَالَ: «وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ، فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْءٍ».


Kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimfikie: 1- “Hakuna siku ambazo matendo mema hupendwa zaidi na Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi,” yaani siku kumi. 2- Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? 3- Akasema Mtume: “Hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu atoke na nafsi yake na mali yake, wala kisirudi chochote


Muhtasari wa Maana

Matendo mema katika siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah si sawa na amali njema katika siku nyingine zisizokuwa siku hizi kumi, isipokuwa mtu atatoka na pesa na maisha yake katika njia ya Mwenyezi Mungu na akauawa kishahidi.

Miradi ya Hadithi