1- Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anafahamisha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alipendelea siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah kuliko siku zingine za mwaka. Malipo ya matendo mema huongezeka maradufu siku hizo, na hakuna amali inayolingana nayo katika siku nyingine.
2- Maswahaba wakasema: Je, jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu si sawa na wema katika siku kumi? Jihad ina malipo makubwa, basi je, matendo haya mema yanafikia kuwa makubwa zaidi katika wema kuliko jihadi?
3- Mtume, Rehema na Amani zimshukie, akawajibu kuwa jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu haifikii wema katika siku hizo kumi, isipokuwa mtu atakayetoka na mali zake na yeye mwenyewe katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha anatumia fedha zake katika kuliweka jeshi, na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka anauawa.
Mafunzo
1- Muislamu atumie fursa ya siku kumi katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu; ina malipo makubwa.
2- Kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu, ametujaalia siku njema katika siku za mwaka ambazo malipo yake yanazidishiwa. Kufunga siku ya Arafa kunafuta madhambi ya miaka miwili, na kufunga siku ya Ashura kunafuta mwaka mmoja, na siku ya Ijumaa kuna saa ya kujibu, na usiku wa cheo ni bora kuliko miezi elfu, na ibada katika kumi za Dhul-Hijjah zina malipo makubwa ya nyongeza, hivyo haifai kwa mtu mwenye akili timamu kupita katika nyakati hizo bila ya kuzidisha ibada.
3- Ni vyema kuchukua fursa ya siku hizo, na mja amkimbilie Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutubia na kurejea Kwake, na kuachana na shirki na maasi.
4- Moja ya ibada bora kabisa anazopaswa kufanya Muislamu katika siku kumi ni kufunga, hasa kufunga siku ya Arafah, ambayo amesema Mtume rehma na Amani zimshukie: “Natumai Mwenyezi Mungu atamsamehe mwaka uliopita na ujao” [1]
5- Muislamu anatakiwa kujiandaa katika siku kumi kwa kufanya tasbiyh na tahlil, Amesema Allah Mtukufu :
“Na litaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku zinazojulikana” ,
na siku zinazojulikana: ni siku kumi, na Mtume amani iwe juu yake, amesema: “Hakuna siku kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, wala zinazo pendeza zaidi kwake kuliko kutenda mema ndani ya siku hizi kumi; Basi zidisha ndani yake tahlil, takbira na kumsifu Allah” [2]
6- Usione haya kuuliza kuhusu dini yako. Maswahabah, Mwenyezi Mungu awawie radhi, hawakuona haya kumuuliza Mtume, rehma na Amani zimshukie, kuhusu ulinganisho wa jihadi na matendo katika hizo siku kumi.
7- Hadithi inajulisha ubora wa jihadi, mpaka Maswahabah waliifananisha na amali zote. Kila Mwislamu anapaswa kuisemesha nafsi yake kuhusu jihad, na kukusudia kufanya jihadi kila inapowezekana, na kutamani kufa kishahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Muislamu hatakiwi kupuuza ibada na utiifu katika siku hizo zilizobarikiwa isipokuwa kwa mtu aliye nyimwa kheri; Amali huongezeka mpaka yasiwe sawa na malipo ya matendo mengine yasiyokuwa katika siku hizo. Basi kutoa sadaka kwa pesa kidogo, rakaa mbili nyepesi, au kufunga siku moja, au kumdhukuru Mwenyezi Mungu kwa maneno bila ya dhiki wala tabu: Haya ni mambo mepesi ambayo hayalingani na amali yoyote isipokuwa mtu anayetoka kwenda jihadi, yeye na mali yake, na kisha anauawa huko.
2.Imepokewa na Ahmad (5446).