عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الأَسْلَمِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «لَا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ القِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ: فِيمَ أَفْنَاهُ؟ وَعَنْ عِلْمِهِ: فِيمَ فَعَلَ؟ وَعَنْ مَالِه: مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ؟ وَفِيمَ أَنْفَقَهُ؟ وَعَنْ جِسْمِهِ: فِيمَ أَبْلَاهُ؟».

Kutoka kwa Abu Barzah Al-Aslamiy, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wasallam:

 1- “Mja hatatembea kusogea mbele Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe

 2- Kuhusu umri wake: Aliumaliza vipi? 

3- Ujuzi wake: alifanya nini? 

4- Kuhusu pesa zake alizipata wapi? Na Alizitumia katika lipi? 

5- Na kuhusu mwili wake: aliuchoshaje? .

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mtukufu:

“Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii” .

[Al-Baqarah: 44]

Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:

“Na humo watapiga makelele: Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema sio yale tuliyo kuwa tukiyafanya. Kwani hatukukupeni umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakujieni Mwonyaji? Basi onjeni! Kwani walio dhulumu hawana wa kuwanusuru”.

[Fatir: 37]

Mtukufu aliye tukuka amesema:

“Na wasimamisheni. Hakika hao ni wenye kuulizwa ” . 

[Al-Saffat: 24]

Na amesema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

“Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa” .  

[Al-Zukhruf: 19]

Mwenyezi Mtukufu amesema:

“Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda” .

[As-Saff: 2]

Miradi ya Hadithi