عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الأَسْلَمِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «لَا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ القِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ: فِيمَ أَفْنَاهُ؟ وَعَنْ عِلْمِهِ: فِيمَ فَعَلَ؟ وَعَنْ مَالِه: مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ؟ وَفِيمَ أَنْفَقَهُ؟ وَعَنْ جِسْمِهِ: فِيمَ أَبْلَاهُ؟».

Kutoka kwa Abu Barzah Al-Aslamiy, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wasallam:

 1- “Mja hatatembea kusogea mbele Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe

 2- Kuhusu umri wake: Aliumaliza vipi? 

3- Ujuzi wake: alifanya nini? 

4- Kuhusu pesa zake alizipata wapi? Na Alizitumia katika lipi? 

5- Na kuhusu mwili wake: aliuchoshaje? .

Abu Barza Al-Aslami

Ni: Abu Barza Al-Aslami Radhi za Mwenyezi Mun-gu ziwe juu yake, Swahaba mkubwa. Alijulikana kwa lakabu yake, na Wanachuoni wametofautiana juu ya jina lake halisi. Ikasemwa: Nadlah bin Ubaid bin Al-Harith, na ikasemwa: Nadlah bin Abdullah bin Al-Harith, ni mmoja katika waliosilimu zamani, alishuhudia kuufungua mji wa Khaybar, kuufungua mji wa Makka na Hunayn, na aliishi mjini Basra. Na aliupiga mji Khurasan, na ndiye aliyemuua Abd al-Uzza bin Khatal chini ya pazia ya Al-Kaaba siku ya ushindi alipoamrisha kuuawa kwake Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alifariki mwaka wa 65. AH


Marejeo

  1. Imepokewa na Al-Tirmidhiy (2417).


Miradi ya Hadithi