عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الأَسْلَمِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «لَا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ القِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ: فِيمَ أَفْنَاهُ؟ وَعَنْ عِلْمِهِ: فِيمَ فَعَلَ؟ وَعَنْ مَالِه: مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ؟ وَفِيمَ أَنْفَقَهُ؟ وَعَنْ جِسْمِهِ: فِيمَ أَبْلَاهُ؟».

Kutoka kwa Abu Barzah Al-Aslamiy, ambaye amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wasallam:

 1- “Mja hatatembea kusogea mbele Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe

 2- Kuhusu umri wake: Aliumaliza vipi? 

3- Ujuzi wake: alifanya nini? 

4- Kuhusu pesa zake alizipata wapi? Na Alizitumia katika lipi? 

5- Na kuhusu mwili wake: aliuchoshaje? .

Muhtasari wa Maana

Mtume Rehma na Amani zimshukie anaeleza kuwa mwanadamu anawajibika kujibu mambo manne; Kuhusu umri wake, elimu, pesa na mwili wake, ni lazima ajitayarishe kwa maswali hayo, na kutumia vitu hivyo kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumpendeza.

Miradi ya Hadithi