عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما، عَنْ رَسُولِ اللهِ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى، قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ، ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا، كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا، كَتَبَهَا اللهُ عَزَّ وَجَلَّ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ، وَإِنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا، كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا، كَتَبَهَا اللهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً».


Kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu yale aliyoyahadithia kutoka kwa Mola wake Mlezi, aliyebarikiwa na aliyetukuka amesema: 1- “Hakika Mwenyezi Mungu aliandika mema na mabaya, kisha akayabainisha. 2- Mwenye kukusudia kufanya jambo jema na asilifanye, Mwenyezi Mungu ataliandika kuwa ni wema kamili. 3- Na akikusudia kulifanya na akalitenda, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humwandikia wema kumi, na humwongezea hadi kufikia mara mia saba, na zaidi ya hayo. 4- Ikiwa alikusudia jambo baya na akawa hakulitenda, basi Mwenyezi Mungu humwandikia jema kamili. 5- Na akikusudia kulifanya na akalitenda, Mwenyezi Mungu huliandika kuwa ni tendo moja baya.”

Muhtasari wa Maana

Katika Hadith, ipo ishara ya ukarimu wa Mwenyezi Mungu na huruma kwa waja Wake. Ambapo huwalipa kwa kutaka kufanya wema, hata wasipofanya, na kuwazidishia malipo ya utiifu kwao, vilevile huwalipa ikiwa watajiepusha na jambo baya wanalokusudia kulifanya. Wakifanya hivyo, huthibitisha kosa moja, bila ziada.

Miradi ya Hadithi