عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما، عَنْ رَسُولِ اللهِ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى، قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ، ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا، كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا، كَتَبَهَا اللهُ عَزَّ وَجَلَّ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ، وَإِنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا، كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا، كَتَبَهَا اللهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً».


Kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu yale aliyoyahadithia kutoka kwa Mola wake Mlezi, aliyebarikiwa na aliyetukuka amesema: 1- “Hakika Mwenyezi Mungu aliandika mema na mabaya, kisha akayabainisha. 2- Mwenye kukusudia kufanya jambo jema na asilifanye, Mwenyezi Mungu ataliandika kuwa ni wema kamili. 3- Na akikusudia kulifanya na akalitenda, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humwandikia wema kumi, na humwongezea hadi kufikia mara mia saba, na zaidi ya hayo. 4- Ikiwa alikusudia jambo baya na akawa hakulitenda, basi Mwenyezi Mungu humwandikia jema kamili. 5- Na akikusudia kulifanya na akalitenda, Mwenyezi Mungu huliandika kuwa ni tendo moja baya.”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mola mlezi Aliyetakasika! “Mfano wa wanao toa mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mafano wa mbegu iliyootesha mashoke saba katika kila shoke, kuna mbegu mia saba, na Mwenyezi Mungu Mtukufu humzidishia amtakaye, na yeye ni mwingi wa kutoa na mjuzi zaidi”.

[Al-Baqara: 261]

Na akasema Mola Mtukufu: “Mwenye kuleta jema atapata mara kumi zaidi yake, na mwenye kuleta ubaya hatalipwa ila mfano wake, wala hawatadhulumiwa”

[Al-An’am. 160].

Na akasema Mwenyezi Mtukufu: “Mwenye kufanya ubaya, basi hatalipwa isipokuwa mfano wake, na anayefanya wema mwanamume au mwanamke, haliyakuwa ni Muumini. Hao wataingia Peponi, wataruzukiwa humo bila hesabu.” .

(Ghafir: 40)

Miradi ya Hadithi