عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ «إنَّ اللَّهَ قَالَ: : مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ: كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنِ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ، وَمَا تَرَدَّدْتُ عَنْ شَيْءٍ أَنَا فَاعِلُهُ تَرَدُّدِي عَنْ نَفْسِ المُؤْمِن، يَكْرَهُ المَوْتَ وَأَنَا أَكْرَهُ مَسَاءَتَهُ» 

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam:

"Mwenyezi Mungu amesema: 1- Yeyote aliye na uadui na rafiki yangu, nimekwisha fanya vita juu yake. 2- Mja wangu hanikurubii na kitu kinachopendwa zaidi Kwangu kuliko nilicho mwajibishia. 3- Na mja Wangu huendelea kujikurubisha kwangu kwa ibada za sunnah mpaka nampenda. 4- Nikimpenda, ninakuwa sikio lake analosikia nalo, macho yake anayotumia kuona, na mkono wake anaopiga nao, na mguu wake anaoutembelea. 5- Akiniomba ninampa, na akiniomba ulinzi namlinda. 6- Na mimi sikusita juu ya jambo lolote ninalofanya huku nikisitasita kama ninavyo sitasita juu ya nafsi ya Muumini, anachukia kifo na mimi nachukia kumkwaza”



Muhtasari wa Maana

Mola wetu Mlezi, ametakasika, anaeleza juu ya utetezi wake kwa mawalii wake, na ukaribu wake kwa waja wake wema, na upendo wake kwao.

Miradi ya Hadithi