عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ «إنَّ اللَّهَ قَالَ: : مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ: كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنِ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ، وَمَا تَرَدَّدْتُ عَنْ شَيْءٍ أَنَا فَاعِلُهُ تَرَدُّدِي عَنْ نَفْسِ المُؤْمِن، يَكْرَهُ المَوْتَ وَأَنَا أَكْرَهُ مَسَاءَتَهُ» 

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam:

"Mwenyezi Mungu amesema: 1- Yeyote aliye na uadui na rafiki yangu, nimekwisha fanya vita juu yake. 2- Mja wangu hanikurubii na kitu kinachopendwa zaidi Kwangu kuliko nilicho mwajibishia. 3- Na mja Wangu huendelea kujikurubisha kwangu kwa ibada za sunnah mpaka nampenda. 4- Nikimpenda, ninakuwa sikio lake analosikia nalo, macho yake anayotumia kuona, na mkono wake anaopiga nao, na mguu wake anaoutembelea. 5- Akiniomba ninampa, na akiniomba ulinzi namlinda. 6- Na mimi sikusita juu ya jambo lolote ninalofanya huku nikisitasita kama ninavyo sitasita juu ya nafsi ya Muumini, anachukia kifo na mimi nachukia kumkwaza”



Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu”

[Al Imran: 31]

Na akasema:

 “Hakika Mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu aliye teremsha Kitabu. Naye ndiye awalindae walio wema” 

[Al-A'raf: 196]

Na Allah jina lake litukuzwe amesema:

“Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika (62) Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Mungu (63) Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa”

[Yunus: 62-64]

Amesema Alla Mtukufu :

. “Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukanya mema”

[Al-Hajj: 38]

Miradi ya Hadithi