عَنْ أَبِي سَعِيدِ بْنِ الْمُعَلَّى، قَالَ: كُنْتُ أُصَلِّي فِي الْمَسْجِدِ، فَدَعَانِي رَسُولُ اللَّهِ ﷺ فَلَمْ أُجِبْهُ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي كُنْتُ أُصَلِّي، فَقَالَ: «أَلَمْ يَقُلِ اللَّهُ: ﴿اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾ [الأنفال: 24]». ثُمَّ قَالَ لِي: «لَأُعَلِّمَنَّكَ سُورَةً هِيَ أَعْظَمُ السُّوَرِ فِي القُرْآنِ، قَبْلَ أَنْ تَخْرُجَ مِنَ المَسْجِدِ». ثُمَّ أَخَذَ بِيَدِي، فَلَمَّا أَرَادَ أَنْ يَخْرُجَ، قُلْتُ لَهُ: «أَلَمْ تَقُلْ: لَأُعَلِّمَنَّكَ سُورَةً هِيَ أَعْظَمُ سُورَةٍ فِي القُرْآنِ؟»، قَالَ: «﴿الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴾ [الفاتحة: 2]، هِيَ السَّبْعُ الْمَثَانِي، وَالقُرْآنُ العَظِيمُ الَّذِي أُوتِيتُهُ».

Kutoka kwa Abu Said bin Al-Mu’alla, Mwenyezi Mungu amuwiye Radhi amesema:

1- Nilikuwa nikiswali msikitini, akaniita Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie lakini sikumjibu. 

2- Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nilikuwa naswali. 

3- Akasema Mtume: “Je, Mwenyezi Mungu hakusema: Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuiteni kwenye yale yanayokuhuisheni” [Al-Anfal: 24]. 

4- Kisha akaniambia: “Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani, kabla hujatoka msikitini.” 

5- Kisha akanishika mkono, na alipotaka kutoka, nilimwambia: “Je, hukusema: Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani” 

6- Akasema: “Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote” [Al-Fatihah: 2], ambazo ni Aya saba zinazorudiwa, na Qur’ani kubwa Tukufu niliyopewa”. 

Muhtasari wa Maana

Hadithi inaonyesha kuwa kuitikia wito wa Mtume Rehema na Amani zimshukie ni wajibu hata kama anayeitwa yuko katika swala, na akaeleza Mtume kuwa Al-Fatihah ni surah kubwa kabisa katika Qur’an.

Miradi ya Hadithi