عَنْ أَبِي سَعِيدِ بْنِ الْمُعَلَّى، قَالَ: كُنْتُ أُصَلِّي فِي الْمَسْجِدِ، فَدَعَانِي رَسُولُ اللَّهِ ﷺ فَلَمْ أُجِبْهُ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي كُنْتُ أُصَلِّي، فَقَالَ: «أَلَمْ يَقُلِ اللَّهُ: ﴿اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾ [الأنفال: 24]». ثُمَّ قَالَ لِي: «لَأُعَلِّمَنَّكَ سُورَةً هِيَ أَعْظَمُ السُّوَرِ فِي القُرْآنِ، قَبْلَ أَنْ تَخْرُجَ مِنَ المَسْجِدِ». ثُمَّ أَخَذَ بِيَدِي، فَلَمَّا أَرَادَ أَنْ يَخْرُجَ، قُلْتُ لَهُ: «أَلَمْ تَقُلْ: لَأُعَلِّمَنَّكَ سُورَةً هِيَ أَعْظَمُ سُورَةٍ فِي القُرْآنِ؟»، قَالَ: «﴿الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴾ [الفاتحة: 2]، هِيَ السَّبْعُ الْمَثَانِي، وَالقُرْآنُ العَظِيمُ الَّذِي أُوتِيتُهُ».

Kutoka kwa Abu Said bin Al-Mu’alla, Mwenyezi Mungu amuwiye Radhi amesema:

1- Nilikuwa nikiswali msikitini, akaniita Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie lakini sikumjibu. 

2- Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nilikuwa naswali. 

3- Akasema Mtume: “Je, Mwenyezi Mungu hakusema: Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuiteni kwenye yale yanayokuhuisheni” [Al-Anfal: 24]. 

4- Kisha akaniambia: “Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani, kabla hujatoka msikitini.” 

5- Kisha akanishika mkono, na alipotaka kutoka, nilimwambia: “Je, hukusema: Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani” 

6- Akasema: “Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote” [Al-Fatihah: 2], ambazo ni Aya saba zinazorudiwa, na Qur’ani kubwa Tukufu niliyopewa”. 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mola Mlezi:

“Enyi mlio amini muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuiteni kwenye yale yanayo kupeni uhai.” .

[Al-Anfal: 24]

Amesema Mwenyezi Mungu:

“Hatufuti wala hatuisahaulishi Aya yoyote, isipokuwa tunaleta iliyo bora zaidi au iliyo mfano wake.” .

[Al-Baqarah: 106]

Akasema Mwenyezi Mungu:

“Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu.” .

[Al-Hijr: 87]

Amesema Mola Mlezi:

Kwa Jina la Mwenyeezi Mungu mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu (1) Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote (2) Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu (3) Mwenye kumiliki siku ya malipo (4) Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada (5) Tuongoe njia iliyonyooka (6) Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea (7) .

[Al-Fatiha]

Miradi ya Hadithi