عَنْ أَبِي سَعِيدِ بْنِ الْمُعَلَّى، قَالَ: كُنْتُ أُصَلِّي فِي الْمَسْجِدِ، فَدَعَانِي رَسُولُ اللَّهِ ﷺ فَلَمْ أُجِبْهُ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي كُنْتُ أُصَلِّي، فَقَالَ: «أَلَمْ يَقُلِ اللَّهُ: ﴿اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾ [الأنفال: 24]». ثُمَّ قَالَ لِي: «لَأُعَلِّمَنَّكَ سُورَةً هِيَ أَعْظَمُ السُّوَرِ فِي القُرْآنِ، قَبْلَ أَنْ تَخْرُجَ مِنَ المَسْجِدِ». ثُمَّ أَخَذَ بِيَدِي، فَلَمَّا أَرَادَ أَنْ يَخْرُجَ، قُلْتُ لَهُ: «أَلَمْ تَقُلْ: لَأُعَلِّمَنَّكَ سُورَةً هِيَ أَعْظَمُ سُورَةٍ فِي القُرْآنِ؟»، قَالَ: «﴿الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴾ [الفاتحة: 2]، هِيَ السَّبْعُ الْمَثَانِي، وَالقُرْآنُ العَظِيمُ الَّذِي أُوتِيتُهُ».

Kutoka kwa Abu Said bin Al-Mu’alla, Mwenyezi Mungu amuwiye Radhi amesema:

1- Nilikuwa nikiswali msikitini, akaniita Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie lakini sikumjibu. 

2- Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nilikuwa naswali. 

3- Akasema Mtume: “Je, Mwenyezi Mungu hakusema: Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuiteni kwenye yale yanayokuhuisheni” [Al-Anfal: 24]. 

4- Kisha akaniambia: “Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani, kabla hujatoka msikitini.” 

5- Kisha akanishika mkono, na alipotaka kutoka, nilimwambia: “Je, hukusema: Nitakufundisha Sura, ambayo ni Sura kubwa kabisa katika Qur’ani” 

6- Akasema: “Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote” [Al-Fatihah: 2], ambazo ni Aya saba zinazorudiwa, na Qur’ani kubwa Tukufu niliyopewa”. 

Abu Saeed bin Al-Mu’alla Mwenyezi Mungu amuwiye Radhi

Ni: Abu Saeed bin Al-Mu’alla Mwenyezi Mungu amuwiye Radhi, ni Sahaba mkubwa, anayejulikana kwa lakabu yake, jina lake katika kauli sahihi ni: Al-Harith bin Nafi’ bin Al-Mu’alla Al-Madani Al-Ansari. Hajulikani miongoni mwa Maswahaba isipokuwa kwa Hadithi mbili: Aliishi Sham, alifariki mwaka wa 73 Hijiria, akiwa na umri wa miaka sitini na nne(1)


Marejeo

  1. Rajea Ufafanuzi Wake katika: “Al-Isti`ab fi Ma`rifat Al-Sahaba” cha Ibn Abd Al-Bar (4/1881), “Asad Al-Ghaba” cha Ibn Al-Atheer (7/186), “Al -Isbah fi Takiz Sahaba” cha Ibn Hajar (8/234)


Miradi ya Hadithi