104 - KUAHACHA BAADHI YA HALALI KWA KUOGOPEA KUINGIA KATIKA HARAMU

عن النُّعْمانِ بنِ بَشيرٍ – رضي الله عنهما - قال: سمعتُ رسولَ اللهِ ﷺ يقول - وأَهْوى النُّعمانُ بإصْبَعَيْهِ إلى أُذُنَيْهِ -: «إنَّ الحَلالَ بَيِّنٌ، وإنَّ الحَرامَ بَيِّنٌ، وبَيْنَهُما مُشْتَبِهاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ،  فَمَنِ اتَّقى الشُّبُهاتِ اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وعِرْضِهِ، ومَن وقَعَ في الشُّبُهاتِ وقَعَ في الحَرامِ، كالرَّاعِي يَرْعى حَوْلَ الحِمى، يُوشِكُ أنْ يَرْتَعَ فِيهِ، ألا وإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى، ألا وإنَّ حِمى اللهِ مَحارِمُهُ، ألا وإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً، إذا صَلَحَتْ صَلَحَ الجَسَدُ كُلُّهُ، وإذا فَسَدَتْ فَسَدَ الجَسَدُ كُلُّهُ، ألا وهي القَلْبُ».

Kutoka kwa Nuuman bin Bashir – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie) akisema – na al-Nu’man aliashiria kwa  vidole vyake kwenye masikio yake:

1. “Halali iko wazi, na haramu iko wazi. 

2. Na kati ya halali na haramu kuna mkanganyiko ambao si watu wengi wanao ufahamu. 

3. Basi mwenye kujiepusha na mashaka atakuwa ameitakasa dhamira na heshima yake ya kidini. 

4. Na anayeingia katika mashaka huanguka katika haramu kama mchungaji anayechunga wanyama wake pembezoni mwa ngome, inakuwa ni karibu zaidi kulisha katika mazao. 

5. Hakika kila Mfalme ana ngome na ulinzi, na hakika ngome ya Mwenyezi Mungu ni mambo yaliyo haramu. 

6. Hakika ndani ya mwili kuna mnofu wa nyama, ukiwa mzuri mnofu huo, basi mwili wote ni mzuri, na ukiharibika mnofu huo mwili wote umeharibika, sasa mnofu huo ndio moyo”

Al-Nu’man bin Bashir bin Saad bin Tha’labah Al-Ansari,

Al-Nu’man bin Bashir bin Saad bin Tha’labah Al-Ansari, mwana wa mfalme, mwanachuoni, swa-haba wa Mtume Rehma na Amani zimshukie na ni mtoto wa sahaba wake. Yeye ni miongoni mwa masahaba vijana kwa makubaliano ya wataalamu wa historia, na alikuwa mmoja wa viongozi wa Muawiyah, na alimteua kwenda Kufa kwa muda, kisha gavana wa wilaya ya Damascus baada ya Fadala. Kisha mtawala wa Homsni mji ulioko kati-kati mwa siria, hadithi zake zilitolewa na maimamu sita katika sunani zao, na hadithi zake ni chache, alikufa katika mwaka wa (64 AH)(1).


Marejeo

  1. 1 Rejea: “Al-Tabaqat Al-Kubra” cha Ibn Saad (6/53), “Al-Isti’ab fi Ma’rifat Al-Ashab” cha Ibn Abd Al-Bar (4/1496), “usdul ghabah” cha Ibn Al-Atheer (4/550).


Miradi ya Hadithi