104 - KUAHACHA BAADHI YA HALALI KWA KUOGOPEA KUINGIA KATIKA HARAMU

عن النُّعْمانِ بنِ بَشيرٍ – رضي الله عنهما - قال: سمعتُ رسولَ اللهِ ﷺ يقول - وأَهْوى النُّعمانُ بإصْبَعَيْهِ إلى أُذُنَيْهِ -: «إنَّ الحَلالَ بَيِّنٌ، وإنَّ الحَرامَ بَيِّنٌ، وبَيْنَهُما مُشْتَبِهاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ،  فَمَنِ اتَّقى الشُّبُهاتِ اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وعِرْضِهِ، ومَن وقَعَ في الشُّبُهاتِ وقَعَ في الحَرامِ، كالرَّاعِي يَرْعى حَوْلَ الحِمى، يُوشِكُ أنْ يَرْتَعَ فِيهِ، ألا وإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى، ألا وإنَّ حِمى اللهِ مَحارِمُهُ، ألا وإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً، إذا صَلَحَتْ صَلَحَ الجَسَدُ كُلُّهُ، وإذا فَسَدَتْ فَسَدَ الجَسَدُ كُلُّهُ، ألا وهي القَلْبُ».

Kutoka kwa Nuuman bin Bashir – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie) akisema – na al-Nu’man aliashiria kwa  vidole vyake kwenye masikio yake:

1. “Halali iko wazi, na haramu iko wazi. 

2. Na kati ya halali na haramu kuna mkanganyiko ambao si watu wengi wanao ufahamu. 

3. Basi mwenye kujiepusha na mashaka atakuwa ameitakasa dhamira na heshima yake ya kidini. 

4. Na anayeingia katika mashaka huanguka katika haramu kama mchungaji anayechunga wanyama wake pembezoni mwa ngome, inakuwa ni karibu zaidi kulisha katika mazao. 

5. Hakika kila Mfalme ana ngome na ulinzi, na hakika ngome ya Mwenyezi Mungu ni mambo yaliyo haramu. 

6. Hakika ndani ya mwili kuna mnofu wa nyama, ukiwa mzuri mnofu huo, basi mwili wote ni mzuri, na ukiharibika mnofu huo mwili wote umeharibika, sasa mnofu huo ndio moyo”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu:

“Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili”.

[Al Imran: 7]

Pia akasema mtukufu:

“Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu

[An Nisaa: 83]

Amesema Mola Mlezi na mtukufu:

“Wala usinifedheheshe Siku watapo fufuliwa (87) Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala watoto (88) Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi”.

[Ash- Shuaraa: 87 - 89]

Miradi ya Hadithi