148 - KUHIFADHI TOBA KWA KUFANYA MATENDO MEMA

عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رضي الله عنه، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ أَشْيَاءَ كُنْتُ أَتَحَنَّثُ بِهَا فِي الجَاهِلِيَّةِ مِنْ صَدَقَةٍ أَوْ عَتَاقَةٍ، وَصِلَةِ رَحِمٍ، فَهَلْ فِيهَا مِنْ أَجْرٍ؟  فَقَالَ النَّبِيُّ : «أَسْلَمْتَ عَلَى مَا سَلَفَ مِنْ خَيْرٍ»

Kutoka kwa Hakim bin Hizam, Allah amuwiye radhi, amesema:

1- Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, unaonaje mambo niliyokuwa nikiyaahidi kabla ya Uislamu, kama vile kutoa sadaka au kuwaacha huru watumwa, kuunga udugu, je nitapata dhawabu? 

2- Akasema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Umeyasilimisha yote yaliyotangulia katika kheri” ).

1- Hakim bin Hizam alimuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu hatima ya matendo mema aliyokuwa akiyafanya kabla ya kusilimu na akikusudia kwayo ibada, kama vile sadaka, kukomboa watumwa, kudumisha uhusiano wa jamaa, na kadhalika. Hakim, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alikuwa mkarimu na mwema. Wakati wa Jahiliyyah aliwakomboa watumwa mia moja na kutoa sadaka ngamia mia moja. Aliposilimu alifanya hivyo hivyo na kusema: “Wallahi mimi siachi chochote nilichokuwa nikikifanya wakati wa Jahiliyyah isipokuwa nitakifanya hivyo katika Uislamu.” [1]

2- Mtume Rehema na Amani zimshukie, akamjibu kuwa amesilimu kwa wema alioufanya. Yaani: Mwenyezi Mungu Mtukufu atakulipa kwa mema uliyoyafanya kabla ya kusilimu kwako, na hatakuadhibu kwa uovu ulioufanya wakati wa ujahili wako.

Mafunzo

1- Hakim, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, hakuona haya kumuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu historia yake kabla ya kusilimu. Kwa hivyo aibu au kiburi visikuzuie kuuliza.

2- Hakim, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alikuwa na shauku ya kutaka kila jambo analolifanya liwe katika mizani ya mema yake, ili ujira wake uwe mwingi sana maradufu na daraja zake zinyanyuliwe. Kwa hiyo hakikisha kwamba kazi yako haijachafuliwa na dosari inayo poromosha matendo mema na kupoteza thawabu yake.

3- Usimzuie kafiri au muovu kufanya jambo jema, kwani anaweza kusilimu na Mwenyezi Mungu Mtukufu amlipe kwa hilo.

4- Tazama rehema kubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na mapenzi yake kwa waja wake. Vipi anawalipa kwa yale waliyoyafanya kabla ya kutubia na kurejea Kwake, na asiwaadhibu kwa makosa waliyoyafanya kabla ya hapo!.

Marejeo

  1.  Imepokewa na Muslim (123).


Miradi ya Hadithi