عَنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «لَا يَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ» وفي رواية: «لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي قَائِمَةً بِأَمْرِ اللهِ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ أَوْ خَالَفَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ عَلَى النَّاسِ»



Kutoka kwa Al-Mughira bin Shu’bah Mwenyezi awe radhi naye kutoka kwa Mtume, amani iwe juu yake, ambaye amesema:

“Kundi la umma wangu litaendelea kushinda mpaka iwafikie amri ya Mwenyezi Mungu na hali wao ni washindi” Na katika riwaya nyengine: “Kundi katika ummah wangu litaendelea kushika amri ya Mwenyezi Mungu, na wale wanaowaacha au kuwapinga hawatawadhuru mpaka ifike amri ya Mwenyezi Mungu”

Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anafahamisha kuwa Dini ya Uislamu itabakia mpaka kitakaposimama kiyama, uislamu utashikwa na wanaume miongoni mwa Waumini watakaosema kwa sauti na kuutetea, na wale wanaopinga au kupigana nao hawatawadhuru.

Miradi ya Hadithi