عَنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «لَا يَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ» وفي رواية: «لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي قَائِمَةً بِأَمْرِ اللهِ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ أَوْ خَالَفَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ عَلَى النَّاسِ»



Kutoka kwa Al-Mughira bin Shu’bah Mwenyezi awe radhi naye kutoka kwa Mtume, amani iwe juu yake, ambaye amesema:

“Kundi la umma wangu litaendelea kushinda mpaka iwafikie amri ya Mwenyezi Mungu na hali wao ni washindi” Na katika riwaya nyengine: “Kundi katika ummah wangu litaendelea kushika amri ya Mwenyezi Mungu, na wale wanaowaacha au kuwapinga hawatawadhuru mpaka ifike amri ya Mwenyezi Mungu”


  1. Anafahamisha Mtume rehma na amani zimshukie kwamba Dini hii itabakia mpaka Siku ya Kiyama, pamoja na kunusurika kwa wale wanaoibeba bendera yake, wakiilinda na kuilingania, kundi la watu katika waislamu litaendelea kuonyesha haki na kuwashinda maadui zao kwa hayo, bila kuficha dini yao, bali wao husema kwa sauti kubwa na hulingania kwenye dini,[1]mpaka ifike siku ya kiyama na ifike amri ya Mwenyezi Mungu, nao wamo katika hali hiyo.

Na maana ya amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni upepo mwema unaokuja kabla ya kiyama hakijasimama, huchukua roho za Waumini; Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Mwenyezi Mungu atatuma upepo kutoka Yemen ambao ni laini kuliko hariri, hautambakisha mtu yeyote mwenye chembe ya imani katika moyo wake.”  [2][3].

2.  Katika riwaya nyingine, Mtume amani iwe juu yake, ameeleza sifa za kundi hilo. Litaendelea kuwepo kundi kwa amri ya Mwenyezi Mungu; Kuamrisha mema na kukataza maovu, kuhukumu sharia ya Mwenyezi Mungu, kueneza elimu kwa watu, na kuwausia Waislamu wanaojishughulisha na kauli ya Mwenyezi Mungu Utukufu ni Wake:

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa”

[Al Imran: 104].

Kundi hili halitadhuriwia kwa kuwa peke yake, au kutokana na watu kutokubaliana nalo, wala halitadhuriwa na wale wataoacha kulisaidia na kulinusuru.

Katika Hadith, kuna dalili kwamba Dunia hii haikosi watu wema walio imara katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu, walio mbali na makatazo Yake, waliohifadhi mambo ya Shari’a. Ni sawa kwao kukubaliana na watu na kutokubaliana nao[4]

Na kundi hili alilolitaja Mtume, amani iwe juu yake, haiko kwenye kundi maalum. Miongoni mwao wamo mafakihi, watu wa Hadith, wasahafu, Mujahidina, na watu wa aina zote za utiifu[5]

Mafunzo

  1. Katika Hadith kuna dalili ya utume wake Mtume, amani iwe juu yake; alipoeleza juu ya kunusurika kwa dini hii, na uimara wa kweli ndani yake mpaka mwisho wa zama, na yale aliyoelezea Mtume, amani iwe juu yake, yalitokea. Hii inathibitisha ukweli wake na huongeza imani juu ya imani yetu.

  2. Usidhani kuwa Uislamu utapungua na kudhoofika mpaka utoweke; Dini ya Mwenyezi Mungu iko dhaahiri na itabakia mpaka kiyama kisimame, na Mwenyezi Mungu ataikamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia.

  3. Walinganiaji na waelimishaji wawatangazie watu yatakayowathibitishia, na waeneze matumaini katika nyoyo zao, kama wanavyowaonya na kuwatahadharisha, na wachanganye baina ya kuwafariji na vitisho, bishara na maonyo.

  4. Jitahidi kuwa miongoni mwa watu wa kundi hilo lenye ushindi, basi shikamana na njia ya uongofu na da’wah, na jihadhari na watu wa upotofu na uzushi.

  5. Hasa lile kundi lililoahidiwa ambalo Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amelisifia kuwa limesimama kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi liweke wewe mwenyewe moyoni mwako na matendo yako, na kisha jiulize Je, wewe ni mmoja wao au la?

  6. Uchache wa wanao elekea kwa Mwenyezi Mungu usikutishe. Kwakuwa wanaofuata haki katika kila wakati na mahali ni wachache, lakini Mwenyezi Mungu huwapa msaada wake.

  7. Muumini wa kweli hayumbishwi na uadui wa watu au upinzani wao kwake. Muumini Lengo lake kuu ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu, hata kama watu wamemkasirikia.

  8. Mwenye hekima na utambuzi anapaswa kushikamana na watu wa kweli na wema kila wakati na mahali popote, afuate njia yao, na awe msaada na nguzo yao.

Marejeo

  1. Tazama: “Fath Al-Bari Sharh Sahih Al-Bukhari” cha Ibn Hajar Al-Asqalani (13/294).
  2. Imepokewa na Muslim (117).
  3. sherh ya An-Nawawi alaa Muslim (13/66).
  4. "Ufafanuzi wa Muraqat al-Mafatih wa Mishkat al-Masabih" na Mulla Ali al-Qari (9/4047).
  5. sherh ya An-Nawawi Alaa Muslim (13/67).

Miradi ya Hadithi