عَنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «لَا يَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ» وفي رواية: «لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي قَائِمَةً بِأَمْرِ اللهِ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ أَوْ خَالَفَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ عَلَى النَّاسِ»



Kutoka kwa Al-Mughira bin Shu’bah Mwenyezi awe radhi naye kutoka kwa Mtume, amani iwe juu yake, ambaye amesema:

“Kundi la umma wangu litaendelea kushinda mpaka iwafikie amri ya Mwenyezi Mungu na hali wao ni washindi” Na katika riwaya nyengine: “Kundi katika ummah wangu litaendelea kushika amri ya Mwenyezi Mungu, na wale wanaowaacha au kuwapinga hawatawadhuru mpaka ifike amri ya Mwenyezi Mungu”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mtukufu: “Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio faulu”

[Al Imran: 104].

Na Amesema Mwenyezi Mtukufu: “Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia (32) 33. Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia”

[At-Tawbah: 32, 33]

Miradi ya Hadithi