عن أبي هُرَيرة رضي الله عنه، قال: قال رسول الله : «تُنْكَحُ الْمَرْأَةُ لأَرْبَعٍ: لِمَالِهَا، وَلِحَسَبِهَا، وَجَمَالِهَا، وَلِدِينِهَا، فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَدَاكَ

Kutoka kwa Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie: “Mwanamke anaolewa kwa sifa nne, kwa pesa yake, kwa nasaba yake, kwa uzuri wake, na kwa dini yake, Basi tafuteni mwanamke aliyeshika dini, mikono yako itakuwa imepatia kuchagua!”

Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anaeleza kuwa watu wanatamani mwanamke aolewe kwa sababu moja kati ya nne; Pesa, nasaba, urembo na dini, na muumini hana budi kuchagua mwanamke kwa ajili ya dini yake; Muumini kufanya hivyo ni bora zaidi kwake na kufanikiwa.

Miradi ya Hadithi