عن أبي هُرَيرة رضي الله عنه، قال: قال رسول الله : «تُنْكَحُ الْمَرْأَةُ لأَرْبَعٍ: لِمَالِهَا، وَلِحَسَبِهَا، وَجَمَالِهَا، وَلِدِينِهَا، فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَدَاكَ

Kutoka kwa Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie: “Mwanamke anaolewa kwa sifa nne, kwa pesa yake, kwa nasaba yake, kwa uzuri wake, na kwa dini yake, Basi tafuteni mwanamke aliyeshika dini, mikono yako itakuwa imepatia kuchagua!”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema

: “Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua”

[An-Nur: 32]

Pia akasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

“Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri”

[Al-Rum: 21]

Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

. “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari”

[Al-Hujraati: 13]

Miradi ya Hadithi