عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال النبيُّ ﷺ: «مَن حَجَّ هذا البيتَ فلم يَرفُثْ، ولم يفسُقْ، رجَعَ كيومِ ولَدَتْهُ أمُّهُ

Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: Amesema Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake: “Mwenye kuhiji kwenye Nyumba hii na wala asifanye uchafu au uovu, atarejea kama siku ile alipozaliwa na mama yake.” 

Muhtasari wa Maana

Hija iliyokubaliwa ni kafara ya madhambi, basi mwenye kuhiji na asifanye chochote kinachoharibu Hijja mfano jimai, dhambi na mengineyo, anarudi kwa familia yake bila ya dhambi kama siku mama yake alipomzaa

Miradi ya Hadithi