عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «إِنَّ الدِّينَ يُسْرٌ، وَلَنْ يُشَادَّ الدِّينَ أَحَدٌ إِلَّا غَلَبَهُ، فَسَدِّدُوا وَقَارِبُوا، وَأَبْشِرُوا،وَاسْتَعِينُوا بِالْغَدْوَةِ وَالرَّوْحَةِ وَشَيْءٍ مِنَ الدُّلْجَةِ»


Kutoka kwa Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, amesema:

1- “Dini ni rahisi, 

2- Hakuna atakayeifanya dini kuwa ngumu ila itamshinda. 

3- Basi semeni kweli na muwaite watu karibu. 

4- Na toeni bishara njema. 

5- Na tafuteni msaada asubuhi na mchana na nyakati za usiku.” .

1.Ametaja Mtume Rehema na Amani zimshukie kuwa Dini ya kweli ya Kiislamu ina sifa ya wepesi katika hukumu zake na urahisi wa gharama zake, kwa hiyo haimshindi mwanadamu, na wala haina gharama nzito ambazo zilikuwepo katika sheria zilizopita; Ilikua kwa Wana wa Israili mtu akifanya dhambi, toba yake kumuua. Na nguo haiwi safi ikipatwa na najisi ila kwa kukata sehemu ya najisi, na ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema katika kumuelezea Mtume Rehma na Amani zimshukie:

“Na Mtume Muhammad anawaondolea mizigo yao ya madhambi na minyororo iliyo kuwa juu yao.”.

[Al-A'raf: 157]

Na wepesi wa Dini ya Kiislamu ni kwamba imeweka masharti ya kuweza

Mtume amani iwe juu yake amesema:

“Niliyokukatazeni jiepusheni, na niliyokuamuruni, fanyeni kadiri muwezavyo” [1]

. si wajibu kwa masikini wenye mahitaji kutoa zaka, bali kwa tajiri ambaye ana miliki kiwango maalumu. Hijja si wajibu ila kwa sharti la kuweza katika fedha, afya na njia, pamoja na swala. Ambapo mtu asiyeweza kusimama anaswali kwa kukaa au kuegemea au apendavyo. Msafiri na mgonjwa hufungua saumu yake kwa ugonjwa unaotegemewa kupona na kisha kuzilipa siku ambazo hakuzifunga, na mgonjwa asiyeweza kufunga kwa vyovyote vile hufungua saumu yake na kumlisha masikini mmoja kwa kila siku, na ndivyo ilivyo katika masuala yote ya kisheria.

Uislamu ndio unaowarahisishia wenye udhuru, kama vile kuhalalisha swala ya khofu kwa wale walio katika vita, kufupisha Swalah na kuunganisha Sala mbili kwa msafiri, na kupangusa viatu kwa muda wa masaa ishirini na nne tu kwa mkazi na kwa msafiri siku tatu mchana na usiku, na mengineyo [2].


2.Hakuna atakayekuwa mkali katika hukumu za Dini na akaacha upole ndani yake na kuwa mkaidi na kujilazimisha asiyoyaweza; Isipokuwa hushindwa. Haijalishi atajidhibiti kiasi gani kwa kutumia nguvu zake na kuwa mvumilivu kwa kile alichojitolea, kuna muda atarudi nyuma na atachoka na kurudi kwenye urahisi. Mwongozo ulio bora kabisa ni uwongofu wa Mtume Rehma na Amani zimshukie na ndio maana aliposema Abdullah bin Amru bin Al-Aas: “Nitakesha usiku na kufunga mchana maadamu ni hai,” Mtume Rehma na Amani zimshukie alipewa habari hiyo, na akamkataza na akamuamrisha kufunga siku tatu za kila mwezi, na kuamka na kulala, lakini Abdullah alikataa kwa kujivunia nguvu na kwamba anaweza kustahimili zaidi, Akasema Mtume Rehma na amani ziwe juu yake: “Funga siku moja na ufungue siku mbili.” Akasema Abdullah bin Amru bin Al-Aas: “Mimi nina uwezo wa kufanya zaidi ya hayo.” Akasema Mtume Rehma na amani ziwe juu yake: “Funga siku moja na ufungue siku moja." Anasema Abdullah bin Amr, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, na baada ya kuwa mzee na kushindwa kushika saumu yake, alisema: “ningezikubali siku tatu alizosema Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, ingependeza kwangu kuliko familia yangu na mali”. [3] ni kwa sababu hakupenda kubadilisha chochote kwa kutengana na Mtume, rehema na amani ziwe juu yake.


3.Ndio maana ni lazima kuwa kati na kati katika ibada, ambayo ni ukati kati ya kupita kiasi na kuzembea, na njia ya kufanya kazi, ambayo ni kwamba ikiwa hatuwezi kuchukua ukamilifu, basi tujitahidi kufanya ibada tuziwezazo kwa karibu zaidi” [4]

Hii ni amri kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani zimshukie) ya kuwa na utaratibu mzuri katika kuabudu bila ya kutia kuzidisha wala kuzembea. Iwapo mtu hana uwezo wa kufanya ibada iliyo bora zaidi, basi afanye ibada yoyote iliyo karibu na yaliyo bora zaidi. Kwa sababu kile ambacho hakipatikani kikamilifu, basi hakiachwi kikamilifu. [5]wakashindwa kufanya ibada kwa njia iliyo bora, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaandalia malipo makubwa bila ya kuwapunguzia ujira wao


4.Kisha Mtume Rehema na Amani zimshukie akawabashiria Ummah wake; Hata wakipungukiwa na vitendo vyao.


5.Na Mtume Rehema na Amani zimshukie alipojua kwamba watu kamwe hawawezi kudumu katika ibada, akawausia kutumia muda wao wa kufanya ibada katika kuMuabudu  Mwenyezi Mungu na kuchunga utiifu wake ambao ndio mwanzo. wa mchana na mwisho wake, na pia akawahimiza kuabudu katika nyakati zinazopendwa na bora zaidi, nayo ni ibada ya mwisho wa usiku [6] .


MAFUNDISHO:


1.Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alitumia herufi “Innaa” ya kufuta, kuashiria uthibitisho na kusadikika kwa maneno yake. Hii ni mojawapo ya mbinu za wasemaji na walinganiaji ambazo walinganiaji wanapaswa kutumia.

2.Iwapo mtu atatafakari juu ya masuala ya kisheria na kuona urahisi na wepesi wake, na ruhusa zinazo patikana kwa wagonjwa na wasiojiweza; Hapo atajua kiwango cha rehema na fadhili za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwa hiyo atazidisha upendo wake kwake na kumridhia kwa kumtii.


3.Hadithi imeeleza kuwa kutokutumia fursa katika kipindi cha dharura kunapelekea mtu kushindwa na kupata hasara, hivyo mja anapohitaji fursa ya ruhusa basi jambo bora na la Sunnah ni kuitumia fursa hiyo na si kujipa uzito, Kila inapokuwa vigumu kwa msafiri kufunga basi afungue saumu, na mgonjwa anapochoka kusimama kuswali basi na aketi, hivyo umasikini na njaa kali ikimpelekea mtu kufikia kula mzoga na vitu vingine ili kuiokoa nafsi yake basi afanye hivyo ili asije kufa [7].

4.Haifai kwa mtu kujitesa katika dini ya Mwenyezi Mungu na kujiwekea uzito kwa kufanya ambayo Mwenyezi Mungu hakumlazimisha, kwa hivyo kujiwekea uzito katika ibada ni kujichosha.


5.Maana ya Hadithi sio kwamba mwenye kujitahidi katika utiifu ni mbaya, lakini jambo baya ni mtu kujiwekea ibada nyingi asizoweza kustahimili.

6.Kushikamana na Sunnah za Mtume (Rehma na Amani zimshukie) ni bora kuliko kuzidisha, kwani kufunga, kula mchana, kusimama usiku kusali na kulala ni bora kuliko kufunga milele na kusimama, na ndio maana Mtume amani iwe juu yake, aliwaambia watu waliosema ibaada ya Mtume (Rehma na Amani zimshukie) na kutaka kuizidisha kwa kusema:

“Wallahi mimi ndio mchamungu wenu na ninaemuogopa Mwenyezi Mungu zaidi kuliko ninyi, lakini pamoja na hayo kuna muda ninafunga na ninakula mchana, na ninasimama usiku na ninalala, na ninaoa wanawake, basi mwenye kujiepusha na Sunnah yangu si katika mimi” [8].

7.Katika Hadithi kuna ushahidi kwamba kufuata sheria ni kuabudu katika mfumo mzuri wa kati na kati; Kwa sababu kujitia uzito na kujitia ngumu kunapelekea kuacha kila aina ya ibada, na dini ni nyepesi, na hakuna atakaye jitilia uzito katika dini isipokuwa itamshinda, na Sharia iliyotakasika imeegemezwa juu ya usahilishaji na kuto kujitenga [9].

8.Inafaa zaidi kwa mfanyakazi kutojituma kwa namna ambayo atashindwa kudumu katika ibada; Badala yake, anatakiwa kufanya ibada kwa upole ili ibada yake idumu na isikatishwe, na katika hadithi:

“Ibada ipendezayo kwa kwa Mwenyezi Mungu Aliye Juu Sana, ni ile inayodumu, hata kama ni ndogo” [10].


9.Kinachotakiwa kwa mja ni kufanya juhudi katika kumtii Mwenyezi Mungu na kutaka kuufikia ukamilifu kadiri awezavyo, anapaswa kujitahidi kuwa mnyenyekevu katika sala, na kuikamilisha ibada kikamilifu, na kuelewa masomo yake yote, na kukaa mbali na dhambi zote na kutekeleza amri zote. Ikiwa, baada ya kujitahidi dhidi ya nafsi yake, atayapata yote, basi ni mwenye kutukuzwa na kulipwa.

10.Sunnah ni msingi wa kati ya vitu viwili ninavyokinzana. Kupindukia na kupita kiasi. Mtu hatakiwi kuzidisha na kutilia ngumu katika ibada, wala asipuuze au kuzembea katika kuacha maamrisho na kufanya mambo ya haramu.


11.Ni katika Sunnah mlinganiaji na faqihi wampe mja mwema bishara ya neema ya Mwenyezi Mungu na malipo ya utiifu wake, na kwamba asikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.

12. Ni lazima mtu achague nyakati nzuri katika kuMuabudu  na kumtii Mwenyezi Mungu. Ikiwa anahisi uvivu au kutojali, anapaswa kulala na kupumzika, kisha aanze tena wakati anapokuwa na nguvu na kuimarika. Atafanya hivyo katika ibada, utiifu, kazi za kidunia, kutafuta elimu, na kadhalika.


13.Jambo zuri ni kuzipangilia ibada kwa mzunguko wa siku nzima ili mtu apate muda mzuri wa utiifu na ibada kuliko kukusanya ibada nyingi kwa saa moja inayochosha mwili.


14.Kutokana na rehema za Mwenyezi Mungu juu yetu, hakutulazimisha kusali swala za usiku, wala hakutuhimiza kuswali usiku mzima, bali Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, amesema katika Hadith: “Na kusinzia kidogo” ili kupunguza na kurahisisha ugumu wa ibada ya usiku, vinginevyo angesema: “Na usiku.”[11]


15.Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume, rehma na amani zimshukie, alikuwa akijiwekea mkeka nyakati za usiku, na anasali usiku. Kisha mkeka huo anaukunjua mchana na kukalia juu yake, hivyo wakawa watu wanashindana kwa wingi kuja kwa Mtume, rehma na amani zimshukie na kusali nyuma yake, Kisha Mtume akaja na kusema: “Enyi watu! fanyeni ibada mnazoziweza, kwani Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke, na matendo yanayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni yenye kudumu hata yakiwa machache."[12]

16.Aliingia Mtume rehma na Amani zimshukie na akaona kamba iliyonyoshwa baina ya nguzo mbili,

akasema Mtume: “Ni kamba gani hii?” Wakasema Maswahaba: Hii ni kamba ya Zainab, na akilegea anaiegemea, basi Mtume rehma na Amani zimshukie akasema: “La, itoweni ili kila mtu afanye ibada kwa uchangamfu wake, na endapo atachoka, mwacheni aketi.” [13].


Marejeo

  1. Imepokewa na Muslim (1337)
  2. Manar Al-Qari Sharh Mukhtasar Sahih Al-Bukhari” cha Hamza Muhammad Qasim (1/121, 122).
  3. Imepokewa na Al-Bukhari (1131) na Muslim (1159)
  4. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (1/95)
  5. Manar Al-Qari Sharh Mukhtasar Sahih Al-Bukhari" cha Hamza Muhammad Qasim (1/123)
  6. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (1/95)
  7. Tazama: Fath al-Bari cha Ibn Hajar (1/ 94, 95)
  8. Imepokewa na Al-Bukhari (5063) na Muslim (1401), kwa kutoka kwa Anas
  9. Nailu al-Awtar" cha al-Shawkani (6/123)
  10. Imepokewa na Al-Bukhari (6464) na Muslim (783), kutoka kwa Mama wa Waumini, Aisha,Mwenyezi Mungu amuwiye radhi
  11. Al-Tafsir Lashrh Al-Jami’ Al-Sahihah” cha Ibn Al-Mulqin (3/87)
  12. (Imepokewa na Al-Bukhari (5861) na Muslim (782
  13. Imepokewa na Al-Bukhari (1150) na Muslim (784), kwa kutoka kwa Anas Mwenyezi Mungu amuwiye radhi.


Miradi ya Hadithi