Mtume (rehema na amani ziwe juu yake) anaeleza ubora wa kutafuta elimu:
1- Akataja kuwa mwenye kufuata njia ya kutafuta elimu yenye manufaa, malipo yake ni kuwa Mwenyezi Mungu atamrahisishia kufanya matendo mema yatakayompelekea kuingia Peponi, na atamuwafikisha katika hilo.
Hadithi hii imetaja njia ya elimu kwa ujumla (Njia. Nlimu); ili ipate Kujumuisha njia zote za kihalisia na kimaana zinazompelekea kuipata elimu, na ili ikusanye aina zote za elimu ya dini na vipengele vyake, na ili kuingia ndani yake elimu kubwa na ndogo.
Mwenye kutafuta elimu anahitajia katika njia yake mambo haya [1]
2- Ameeleza Mtume Muhammad (s.a.w) kwamba: Malaika wanafunika mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu, ima kwa kumnyenyekea, na kutukuza thamani yake, au malaika huweka mbawa zao, wanaacha kupaa na kuruka na wanateremka kwa mwenye kutafuta elimu, kisha wanamfunika na kumwekea kivuli mwenye kutafuta elimu.
Kama alivyosemaMtume muhammad (s.a.w):
“Hawakai watu wakimtaja Mwenyezi Mungu Aliye takasika na kutukuka, ispokuwa malaika wanawafunika watu hao” [2]
3- Kisha akataja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) fadhila nyingine nyingi kwa ajili ya mwenye kutafuta elimu. " Na mwenye kutafuta elimu ya kisheria hakika Mwenyezi Mungu mtukufu anavidhalilisha viumbe vyote kwa ajili ya kumwombea msamaha mwenye kutafuta elimu ya sheria na vinamuombea dua; kwani athari za elimu yake na matendo yake ni sababu ya kuteremka rehma za Allah kwa walimwengu kwa sababu wingi wa utiifu kwa Mwenyezimungu (s.w) “[3] . Na kwa hakika miongoni mwa dalili za kusimama qiyama ni kuondolewa elimu ya kisheria na kuenea ujinga, nayo ni dalili juu ya kukaribia kuangamia. Na hii fadhila ni kama maneno ya Mtume
“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake na viumbe wa mbinguni na ardhini mpaka mdudu chungu katika shimo lake na hata samaki, wote hao wanamwombea dua anaewafundisha watu mambo ya kheri” [4]
4- Na akataja kwamba mjuzi ambaye atatekeleza haki ya elimu kwa kuifanyia kazi na kuisomesha anakua mbora zaidi kuliko mwenye kusali tu ambaye amejitenga na watu kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu, ni kama ubora wa mwezi pamoja na nyota; kwani mwezi unaangaza mbali zaidi, wanaongoka kwa nuru yake wasafiri wawapo jangwani, na miji inanufaika kwa nuru hiyo miji na waja, wakati nuru ya nyota inaishia kwenye nyota zenyewe,wala nuru ya nyota haivuki kuangazia kutu kingine ambacho kipo pembeni yake, basi hivyo ndivyo ilivyo kwa mjuzi na mfanya ibada; mjuzi (msomi) akamnufaisha mwingine, lakini ibada ya mwenye kuabudu yainaishia malipo yake kwake tu.
Na huenda Mtume wa Mwenyezimungu mtukufu (s.a.w) alimfananisha mwanazuoni na mwezi tofauti na jua kwa mfano; ni kwa sababu nuru ya mwezi ilipokua yenye kunufaisha kitu kingine- nalo ni jua- hakika amemfananisha mwanachuoni ambaye ilinufaisha nuru yake kutoka katika nuru ya utume: kutoka katika ufunuo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na mafundisho ya Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake.
5- Kisha akataja fadhila nyengine kwa wanavyuoni, na akataja kuwa wao ni warithi wa Mitume.Wanachuoni ni kama watoto kwa Mitume, na kama ambavyo watoto wa mtu wanarithi mali yake baada ya kufa kwake, basi wanachuoni ndio wanaorithi ujuzi wa manabii, wanauchukua ujuzi huo kutoka kwao, na wanaueneza kwa watu; Na kwa sababu manabii hawakurithisha dinari ya dhahabu, au dirhamu ya fedha, au aina yoyote ya fedha; Bali wamerithi elimu, basi aliyeichukua ametwaa bahati kubwa zaidi ya fedha, na amechukua fungu kamili katika urithi wa unabii.
1. Kila nafsi yako ikitamania pepo, au ikiwa nzito kuitafuta pepo basi fanya hima kuitafuta elimuya kisheria, kwani elimu yenyewe ni ibada, na hiyo elimu ndio inakubainishia ni ibada ipi yenye malipo makubwa, na yenyewe inaingiza katika nafsi nashati na uchangamfu na kuridhika na kusubirijuu ya ibada.
2. Yeyote mwenye kutaka daraja la juu na Baraka na wepesi wa mambo yake basi atafute elimu ya kisheria, kwani hakika malaika –na wao ni miongoni mwa viumbe vitukufu alivyoviumba Mwenyezi Mungu (s.w)- wanawakirimu wanaotafuta elimu ya kisheria, na wanawazunguka, na wanatekeleza anayo waamrisha Mwenyezi Mungu (s.w) kurahisisha mambo yao.
3. Ni juu ya anaye tafuta elimu kuithamini na kuiheshimu elimu, kwani hakika Mwenyezi Mungu mtukufu anao malaika waliowakilishwa katika vikao vya wanazuoni, na ni juu yake kuwaheshimu malaika, ajiepushe katika kikao chake kuwepo mbwa au picha, na atambue hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amewawakilisha kwake Malaika wema, wakidhibiti kila kitu na wakiandika.
4. Ni wingi ulioje wa madhambi yetu! na tunapohitajia kuomba msamaha kwa wingi kama tulivyo fanya madhambi kwa wingi, basi katika elimu na kuieneza kunapatikana sababu za kuombewa msamaha na viumbe wa mbinguni na ardhini kwetu, wakiwemo kati yao ni waja wema.
5. Huu ulimwengu ambao unaudhania kuwa haubadiliki, unaishi pamoja na Mwenyezi Mungu mtukufu, basi hata samaki ambao unawadhania kuwa hawaongei nao wanamtakia msamaha mwenye kuitafuta elimu kwa idhini ya mola wao ambaye kila kiumbe amekipatia umbile lake na akakiongoza.
6. Mwenyezi Mungu amemfadhilisha mwenye elimu juu ya mfanya ibada kwa kuwa mjuzi anakuwa na nuru kama mwezi ambayo anaisambaza kwa watu, ama akijificha na watu, na akafanya ubahili kwa elimu yake, au akawa mzito kuitoa, na akaridhika kufunikwa na maafa: kwa hali hiyo ubora wake utapatikana wapi dhidi ya watu wengine?
7. Hadithi hii inabainisha kuwa watu wakubwa katika daraja ni wanachuoni. Kwani wao ndio warithi wa watu bora na watukufu zaidi, na baada ya Mitume hakukuwa na mtu yeyote aliyepeleka ujumbe wao duniani anayestahiki zaidi ya wenye elimu, na kwa ajili hiyo wao ndio watu bora zaidi baada ya Mitume. Na hii thamani laiti mtu angeijuwa angepambana na starehe za dunia na vikwazo vyake kwa ajili yake.
8.
Katika kauli yake Mtume (s.a.w):
“Hakika mitume hawakurithiwa dinari wala dirham” hiyo ni dalili tosha ya kukinai kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu mtukufu, rehma na amani ziwe juu yao, katika starehe ya dunia yenye kuondoka .[5]
9. Wanazuoni ndio warithi wa mitume, na hakika wamewarithi na subra juu ya elimu na kuieneza. Hakika alisafiri Nabii mussa (a.s) na akaivumilia njaa kwa ajili ya kutafuta elimu kwa mtu ambaye yuko chini yake ambaye ni Alkhidhri, na alivumilia (s.a.w) maudhi katika kuieneza elimu, hiyo ndio hali ilivyo kwa warithi wa mitume. Na katika mfano mzuri katika hayo, hakika ibn abiy hatim al-raziy alisema: “Tulikuwa katika Nchi ya misri kwa muda wa miezi saba hatukula katika kipindi hicho murqat (chakula chenye mchuzi) mchana wetu tunaumaliza tukiwa kwa masheikh zetu, na usiku tunahamisha (tunaandika) na kubadilishana, siku moja tukamwendea sheikh wetu mimi na rafiki yangu,wakatueleza kuwa sheikh ni mgonjwa, basi nikamuona samaki aliye tuvutia tukamnunua,, na tulipofika nyumbani ukawa ni muda mwingine wa kuhudhuria darasa kwa masheikh zetu, tukaondoka, basi alibakia samaki Yule siku tatu,na alikaribia kabisa kuoza, tukamla akiwa kaharibika kwani hatukupata muda wa kumwandaa vizuri” kisha akasema: “ haipatikani elimu kwa kuupa starehe mwili”. [6]
10. Anapo taka mtu kumuogopa Mwenyezi Mungu ukweli wa kuogopa kwake, basi nijuu yake kujifunza elimu (kusoma elimu ya dini); kwa sababu mwenye kujinza elimu ya kisheria basi atajuwa thamani na utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Na kwa ajili hiyo amesema allah mtukufu:
“Hakika katika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu ni wanazuoni” .
Ametumia kudhibiti kwa innamaa (yaani si vinginevyo), kama kwamba amesema: Hakuna yeyote anaemuogopa Mwenyezi Mungu isipokuwa wanazuoni; kwa sababu woga wao ni woga wa kweli unaotokamana na elimu yao wanavyomjuwa Mwenyezi Mungu.
11. Amesema mshairi:
Itakapo kuwa elimu yako haijakunufaisha kwa kheri yoyote = basi bora zaidi kwako usingelikuwa na elimu
Na ikiwa uelewa wako utakuingiza katika upotevu = basi afadhali wewe tena afadhali zaidi usingekuwa na uelwa
Utavuna ujinga kutokana na matunda ya kusalenda = na utabaki kuwa dhalili kwa watu pindi ukiwa mkubwa.
Marejeo
- Muslim (2700), kutoka kwa Abu Hurairah na Abu Said al-Khudri, Mungu awe radhi nao.
- Tazama: Fath al-Bari Ibn Hajar (1/160)
- Tazama: “Sharh Riyadh as-Swalihin ya Ibn Uthaymiyn” (5/433-434).
- Al-Tirmidhiy (2685), kwa kutoka kwa Abu Umamah Al-Bahili, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na Al-Tirmidhiy amesema: Ni nzuri na sahihi.
- Sharh ya al-Tibi katika kitabu cha Mishkat al-Masabih (2/673).
- Al-Tirmidhiy (2685), kutoka kwa Abu Umamah Al-Bahili, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na Al-Tirmidhiy amesema: Ni nzuri na sahihi.