عن أبي الدَّرْداءِ قال: سمعتُ رسولَ الله ﷺ يقولُ: «مَن سلَكَ طريقًا يَلتمِسُ فيه عِلمًا، سهَّلَ اللهُ له طريقًا إلى الجنةِ، وإنَّ الملائكةَ لَتضَعُ أجنحتَها رضًا لطالب العلم، وإنَّ طالبَ العلم يَستغفِرُ له مَن في السماء والأرض، حتى الحيتانُ في الماء، وإنَّ فضلَ العالِم على العابد كفضل القمرِ على سائر الكواكب، وإنَّ العلماءَ ورَثةُ الأنبياء، وإنَّ الأنبياءَ لم يورِّثوا دينارًا ولا درهمًا؛ إنما ورَّثوا العلمَ، فمَن أخذه أخَذ بحظٍّ وافرٍ».

Kutoka kwa Abuu Dar-Dai (r.a) amesema: nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake akisema:

1. “Mwenye kupita njia akitafuta elimu katika njia hiyo, Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi zaidi njia ya kwenda peponi. 

2. Na hakika malaika naapa kwa Allah wanaweka mbawa zao kumridhia mtafuta elimu,  

3. Na hakika mwenye kutafuta elimu wanamuombea msamaha viumbe wa mbinguni na ardhini, hata pia samaki katika maji. 

4. Na hakika ubora wa mwanazuoni kwa waja wa Mwenyezi Mungu ni kama ubora wa mwezi juu ya nyota zote. 

5. Na hakika wanazuoni ndio warithi wa mitume wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na hakika mitume wa Allah hawakurithiwa dinari wala dir-ham; bali si vinginevyo walirithiwa elimu, basi atakeichukuwa atakua amechukua fungu kubwa sana. 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

7. " Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.

[surat Al Imran: 7]

 Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

18. Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana Mola muabudiwa kwa haki ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana Mola muabudiwa kwa haki ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima”. .

[Surat Al Imran: 18]

43. "Na hiyo ni mifano tunawapigia watu, na hawaifahamu ila wenye elimu”. .

[surat Surat Al-Ankabut: 43]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

" Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni ". .

[surat Fatir: 28]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

9. "Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi...Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili ".  .

[surat Al-Zumar: 9]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

11. " Enyi mlio amini! Mkiambiwa: Panueni nafasi katika mabaraza, basi panueni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: Ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda ".

[surat Al Mujaadalah: 11]

Miradi ya Hadithi