عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ بَعَثَهُ إِلَى اليَمَنِ، فَسَأَلَهُ عَنْ أَشْرِبَةٍ تُصْنَعُ بِهَا، فَقَالَ: «وَمَا هِيَ؟» قَالَ: البِتْعُ وَالْمِزْرُ، فَقُلْتُ لِأَبِي بُرْدَةَ: مَا البِتْعُ؟ قَالَ: نَبِيذُ العَسَلِ، وَالْمِزْرُ نَبِيذُ الشَّعِيرِ، فَقَالَ: «كُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ»

Kutoka kwa Said bin Abi Burdah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abi Musa Al-Ash’ariy Mwenyezi Mungu awe radhi nao, 1. Mtume rehma na Amani zimshukie alimtuma Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji vinavyotengenezwa huko, akasema: “Ni nini? Akasema: Al-bit’u na Al-mizru, basi nikamwambia baba Burdah: Al-bit’u ndio nini? Akasema: mchanganyo wa asali, na Al-mizru, ni mchanganyo wa shayiri. 2. Akasema: “Kila kilevi ni haramu”

 


Muhtasari wa Maana

Sababu ya uharamu wa mvinyo ni kwamba husababisha ulevi na kuifanya akili kwenda mbali. Kila kinachoifanya akili kwenda mbali ni haramu, iwe ni zabibu au kitu kingine.

Miradi ya Hadithi