عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ رضى الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ قَالَ: «الدِّينُ النَّصِيحَةُ»، قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلَّهِ، وَلِكِتَابِهِ،وَلِرَسُولِهِ،وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ، وَعَامَّتِهِمْ»


Kutoka kwa Tamim al-Dari (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yakr) kwamba Mtume (Rehma na Amani zimshukie) amesema:1."Dini ni kunasihiana" 2.  Tukasema:

Kwa ajili ya nani? 3.Akasema: “Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,4.Na kwa kitabu chake. 5.Na kwa Mtume wake. 6.Kwa viongozi wa Waislamu. 7. Na watu wote”.

Abu Ruqayya Tamim bin Aws

Abu Ruqayya Tamim bin Aws bin Khaarija Al-Dari (babu yake ambaye jina lake ni Al-Dar) kutoka kabila la Lakhm. Swahaba huyu Alikuwa Mkristo katika watu wa siria, alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake), mwaka wa tisa hijiriya akaingia katika Uislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu akampa waqfu wa ardhi katika mji wa habron na akamtapia bustani ya Beit Ainun huko parestina. Tamim aliambatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Alipigania dini pamoja na Mtume, na alipokea hadithi kutoka kwake, na akakaa Madina kisha akaenda siria, alifariki huko Palestina mwaka wa 40 Hijiria

Miradi ya Hadithi