18 - KUTUTWA UTUME KWA UJIO KWA NABII MUHAMMAD (S.A.W)

عن أبي هريرة أن رَسُول اللهِ قال: «وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لا يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلا نَصْرَانِيٌّ، ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ: إِلَّا كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ» رواه مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehme na Amani zimfikie) amesema:

-:Naapa kwa Yule Ambaye nafsi ya Muhammad Iko Mikononi Mwake. Hakuna hata mmoja katika Umma Huu atakae sikia ulinganizi wangu.Awe Myahudi au Mnaswara (Mkristo)Kisha akafa bila ya kuyaamini niliyotumwa nay o, isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.”

Imepokewa na Muslim.

 

  1. Mtume (Rehme na Amani zimfikie), ameapa kwa Mwenyezi Mungu akithibitisha jambo kubwa, akasema: Wallahi naapa kwa yule ambaye uhai na nafsi yangu vipo mikononi mwake, Akitaka ananifisha na akitaka anaipa uhai.

  2. Maudhui ya kiapo hiki yanazungumzia wajibu wa kuamini kwa wale wote waliofikiwa na wito wa Mtume (rehme na Amani zimfikie); katika ummah aliyotumwa kuwafikishia watu na majini, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, tangu zama zake mpaka siku ya Qiyaamah. Na kufika kwa wito huo kunakokusudiwa ni ufahamu wa mwenye kuwajibikiwa (yaani aliebalehe) kuwa yupo Mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Analingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kukataza ushirikina, na kuyabainisha hayo yote na mengine mengi, sawa sawa awe amekinai katika hoja au asiwe amekinai, ile kufahamu ufahamu sahihi kuwa yupo Mtume mwenye sifa maalumu aliyetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu unamtosheleza kusimamishiwa hoja dhidi yake. Na ama yule ambaye hakufikishiwa ujumbe kwa usahihi, hatusemi kuwa mtu huyu atasimamishiwa hoja dhidi yake, Kwani Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Na hatukuwa ni wenye kuadhibu, mpaka tumtume Mjumbe”

    [Al-Isra: 15].

  3. Mtume (Rehme na Amani zimfikie), amewataja Mayahudi na Manasara kwa sababu wao ndio watu wanaomfahamu zaidi Mtume Muhammad (Rehme na Amani zimfikie) na habari njema za utume wake ziliwajia kabla ya ujio wake, Pia kuwataja wao kunaashiria kwamba imani yao ya kuamini dini zilizotoka mbininguni haitaafaa kwa chochote baada ya ujio wa Mtume wa mwisho ambae ni Muhammad (Rehme na Amani zimfikie). Halikadhalika wapagani (wasiokuwa na dini) na wasioamini Mwenyezi Mungu wote wanaingia katika hukumu hiyo. Na hii ni ushahidi kwamba sheria ya za Mtume (Rehme na Amani zimfikie) zilifuta sheria zote zilizokuwa kabla yake.). [1]

  4. Kila mtu mzima mwenye akili timamu aliyefikiwa na wito huo (wa uislamu), kisha akafa bila kuamini ujumbe wa Mtume wa mwisho wala hakufuata sheria aliyoileta, basi atakuwa miongoni mwa watu wa Motoni atakaa humo milele, hayatamfaa matendo, nasaba, heshima wala hadhi yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake, na Akhera atakuwa miongoni mwa walio pata hasara”

    [Al Imran: 85].

Mafunzo

Tunajifunza katika hadithi yafuatayo: -

  1. Abu Huraira (Mwenyezi Mungu amuwie radhi) alivuka umbali mrefu kutoka katika Mji wake, na akaridhia kukabiliana na misukusuko ya kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwani ilikuwa inatosha kwake kusilimu katika Mji wake, na akabaki huko huko, bali alihama na kusuhubiana na Mtume (Rehme na Amani zimfikie) hadi akawa ni mpokezi na msimulizi wa Hadith nyingi, licha ya kuwa kusilimu kwake kulikuwa si zaidi ya miaka takribani mitatu tu, basi kila mmoja wetu ajitazame mwenyewe na kujiuliza maswali haya,  je nimefanya nini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Na nina pupa (hamasa) kiasi gani katika kufuata mwenendo wa Mtume (Rehme na Amani zimfikie) ambao ndio urithi wetu.

  2. Tunajifunza katika hadithi hii kuyatukuza mambo ya Imani, na tunyenyekee kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehme na Amani zimfikie) katika kila jambo alilotuamrisha, sawa sawa liwe linaendana na Matamanio yetu au liko tofauti. Kwa kusisitiza hilo Mtume (Rehme na Amani zimfikie), ameapa kwa yule ambaye uhai na kifo chake vimo mikononi mwake, juu ya mambo ya imani.

Mwenye undugu au Uhusiano na Myahudi au Mkristo basi amfanyie wema kwa kumlingania kwenye Uislamu, kwani dini yake haimfai kwa chochote, na akisilimu ana malipo mara mbili, Amesema Mtume (Rehme na Amani zimfikie): “Watu wa aina tatu watapata malipo mara mbili: (katika moja ya watu hao mtume akataja) Mtu katika Ahlul-Kitab (yahudi au naswara) atakayemuamini Mtume wake na kumuamini Nabii Muhammad (Rehme na Amani zimfikie)”[2]

Muislamu anapaswa kujivunia na kujifaharisha na dini yake, Fahari inayozidi fahari ya mwenye kujivunia mali na maendeleo yake, kwani wafuasi wote wa dini nyingine wanapata hasara kubwa kama hawatofuata dini ya Kiislamu pindi unapawafikia ulinganizi wake. Hakika Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuwa Waislamu, na akatuongoza kuifuata haki na kushikamana nayo.

  Huruma  kubwa zaidi ni mtu kuihurumia nafsi yake na nafsi za ndugu na jamaa zake kwa kujitahidi kuziokoa  katika adhabu ya milele, kwani mtu yeyote hataingia Peponi mpaka amuamini Mtume (Rehme na Amani zimfikie) na awe ameamini ujumbe wake na kumfuata, na wanaolingania katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio watu wenye huruma zaidi, kwani Wanajitahidi kulingania kwa ndimi zao, fedha, na elimu alizowapatia Mwenyezi Mungu  ili kuwatoa watu katika adhabu ya Mwenyezi Mungu, hakika katika jukumu hilo kuna hadhi na cheo kikubwa ambacho kila Mwislamu anatakiwa kuwa nacho, kwa kuwa na tabia ya kulingania katika njia ya  Mwenyezi Mungu Mtukufu. 

Amesema mshairi:

Fuata mwenendo wa mbora wa viumbe, kwani ndio njia ya kuwaokoa wanadamu.

neema zake zimekienea kila kiumbe = na wema wake umetawala duniani na akhera 

Alipokuja Mtume watu waliiona haki = na wakayaandaa masikio yao kuisikiliza.

Ewe Mola, mpe baraka ya kila tone la mvua inyeshapo, na Baraka ya kila yakimea majani na matawi.

Na umpelekee amani yenye harufu nzuri = Na familia na Maswahaba muda wote.

Marejeo

  1. Tazama: “Tuhfat al-Abrar” cha al-Baidawi (1/43), “Al-Maftahat fi Sharh al-Masabih” cha al-Mazhari (1/72).
  2.  Imepokewa na Al-Bukhari (97) na Muslim (154), kwa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ariy 




Miradi ya Hadithi