عن عبدِ الله بنِ عمرٍورضي الله عنه عن النبيِّ ، قال:«أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقًا خَالِصًا، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَهَا:إِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ،وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ،وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ» متفق عليه

Kutoka kwa Abdullah bun Amri, kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), amesema:

1.    “Mambo manne anaye kuwa nayo anakuwa ni mnafiki halisi, na anaye kuwa na moja wapo, anakuwa na sifa ya kinafiki mpaka ayaache; 2.Anapo aminiwa, anafanya hiyana 3.Anapo ongea hudanganya 4.Anapo ahidi, husaliti 5.Anapo kosana na mtu, anavuka mipaka.


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mola mlezi:

“Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo toa hukumu kati ya watu basi mtowe hukumu kwa uadilifu”

[An-Nisa: 58].

Na akasema aliye mtuklufu:

“Hakika wanaafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni, wala hautowapatia yeyote wa kuwanusuru (145) Isipo kuwa wale walio tubu, na wakatengeneza na wakashikamana na Mwenyezi Mungu, na wakaitakasa Dini yao kwa Mwenyezi Mungu. Basi hao watakluwa pamoja na Waumini. Na Mwenyezi Mungu atakuja wapa Waumini ujira mkubwa” .

[An-Nisa: 145, 146]

Amesema mwenyezi mufu:

“Enyi mlio amini! Timizeni ahadi”

[Al- Maaidah: 1].

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu”

[Al- Maaidah: 8].

Amesema Mola mlezi, majina yake yametakaswa

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli” .

[At-Tawbah: 119]

Miradi ya Hadithi