عن عبدِ الله بنِ عمرٍورضي الله عنه عن النبيِّ ، قال:«أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقًا خَالِصًا، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَهَا:إِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ،وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ،وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ» متفق عليه

Kutoka kwa Abdullah bun Amri, kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), amesema:

1.    “Mambo manne anaye kuwa nayo anakuwa ni mnafiki halisi, na anaye kuwa na moja wapo, anakuwa na sifa ya kinafiki mpaka ayaache; 2.Anapo aminiwa, anafanya hiyana 3.Anapo ongea hudanganya 4.Anapo ahidi, husaliti 5.Anapo kosana na mtu, anavuka mipaka.



Unafiki ni katika maradhi hatari yanayo  mpata mtu mmjo mmoj na jamii kwa ujumla, ndio maana uislam ukatadharisha sana na kubainisha sifa za wanafiki, ili muumini achukue taahadhari, na ajichunge asije kusifika kwa tabia zao. 

1.Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amewatajia maswahaba zake sifa nne ambazo hasifiki nazo mwislam, bali ni za mnafiki, mtu anapo kuwa nazo zote, nakuwa mnafiki kikamilifu.

Unafiki; ni mtu kudhihirisha kinyume na alicho nacho moyoni, na unagawanyika mara mbili; unafiki wa itikadi; ni mtu kudhihirisha uislam na kuficha ukafiri, huu unamtoa katika uislam.

Na hao Mwenyezi Mungu amewasema katika kauli yake:

““Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni, wala hautowapatia yeyote wa kuwanusuru (145) Isipo kuwa wale walio tubu, na wakatengeneza na wakashikamana na Mwenyezi Mungu, na wakaitakasa Dini yao kwa Mwenyezi Mungu. Basi hao watakluwa pamoja na Waumini. Na Mwenyezi Mungu atakuja wapa Waumini ujira mkubwa” .”

[An-Nisa: 145, 146]

. aina nyingine ni unafiki wa matendo; kama uongo na kusaliti, kama ilivyo tajwa kwenye Hadithi. Huu haumtoi mtu katika Uislam, lakini ana kuwa na sifa miongoni mwa sifa za kinafiki, na mwenye nazo anafanana na wanafiki na ameahidiwa adhabu ya Moto

akesema:

“jiepusheni na uongo kwani uwongo unampelekea katika uchafu na uovu, na uovu unapelekea kuingia Moto, na mtu atasema uongo mpaka aandikwe kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mwongo."[3]”.

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliona katika ndoto mtu anavuta mdomo wake mpaka kwenye kisogo na kuujeruhi, na pua lake mpaka kwenye kisogo na kulijeruhi na macho yake mpaka kwenye kisogo na kuyajeruhi, akauliza, akaambiwa: ni mtu anaeongea uongo unachukuliwa mapaka unaenea sehemu mbali mbali”[4].

5.Sifa ya tatu: ni kusaliti makubaliaono. Anapo weka ahadi ya makubaliano na mtu anamhadaa kwa kumsaliti. Mwenyezi Mungu ameharamisha usaliti na ameukataza sehemu zaidi ya moja katika Qur`ani.

Amesema Mtukufu:

““Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo” ”.

[An-Nahl: 91]

Na akesema Mtukufu:

“Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa”

[Al-Isra: 34]

6.Sifa ya nne: ni mtu kuiacha haki katika ugomvi, na kutumia hila kuirudisha na kujaribu kuchukua ambacho si haki yake, hasa  anapokuwa na uwezo wa kuongea na kusimamishaa hoja.

Mwenyezi Mungu amewaamrisha waja wake uadilifu katika kila jambo, na akawazuia wasisukumwe na chuki za ugomvi wakadhulumu upande fulani

amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu”

[Al- Maaidah: 8].

Na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ameeleza hatima mbaya ya anae chukua haki ya mwenzake kwa dhuluma, akasema: “hakika nyinyi mnashtakiana kwangu, huenda baadhi yenu wakawa na ufasaha wa uwasilishaji wa hoja zao kuliko wengine, nikahukumu kuwa ameshinda kwa mujibu wa nilivyo sikia, yeyote ambaye nitampa haki ya mwenzake hata kidogo, basi asiichukue, nitakua namkatia sehemu katika Moto”[5] Mambo haya manne yanakusanya misingi ya unafiki, na kuna sifa nyingine ambazo zinatokana na hizi, kama kutotekeleza ahadi[6]. Alama za unafiki na sifa zao ni nyingi, asili yake ni hizo, inatakiwa mwislam ajitahidi asiwe na sifa yoyote katika hizo.

MAFUNDISHO

1.Miongoni mwa njia nzuri za Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) za kufundishia, ni kusogeza mukusudio kwa kutumia njia mbali mbali, kama vile idadi. Mwislam anapo sikia kwamba sifa zitakazo tajwa ni nne, anapata hamu ya kuzisikia na kuzikalili. Inatakiwa wasomi na wanao lingania watumie njia kama hizi wakiwa wanazungumza na watu 


2.Unafiki ni sifa mbaya sana, na kila sifa yake pia ni mbaya, aliye mkweli na ana anajitambua hujiepusha na sifa hizo na wala hajitakasi, amesema Ibun abii Mulaikah -miongoni mwa wanafunzi wa maswahaba-: “niliwadiriki  maswahaba thelathini wa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), wote wanaogopa unafiki usije ukawapata, hayupo anae sema: yeye ana Imani kama ya Jibril na Mikael”[7].


3.Inatakiwa ewe mwenye majukumu, uwe makini na amana unazo kabidhiwa. Sawa sawa kutoka kwa wazazi au wakubwa wako kazini, au marafiki zako, ukihitajia kuandika ili usisahau, au usipoteze, basi andika. Baadhi ya wema walio tangulia walikuwa wakidhibiti kila amana hata kama ni kalamu, au pesa ndogo ya mtoto.


4.Kutekeleza amana ni miongoni mwa sifa nzuri, washirikina katika mji wa Makka walikuwa wakimuita Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) Muaminifu, kwa sababu ni jambo linalo hitaji kujikaza, umakini na kupupia, jitahidi uwe hivyo.

5.Jizoeshe kuwa mkweli hata kama ni katika mambo madogo, tabia ya ukweli ni mazoea, usiseme uongo kwa kisingizio cha mzaha, au kuliwazana, au maslahi, jambo hili halihitaji vitu kama hivyo. Mtu anakuwa na tabia ya uongo mpaka inakita katika damu yake, inakuwa ni kazi kuiacha, kiasi cha kujulikana kwa tabia hiyo katika jamii. Inasimuliwa kwamba Abuu Sufiyaan alitaka kumndanganya Hiraqil kuhusu Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), lakini aliacha, na alikuwa bado ni kafiri.


6.Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ameamrisha kutekeleza ahadi hata kama ni washirikina tena katika kipindi cha vita. Hudhaifa bun Yamaan na baba yake, walikuja kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) katika kipandi cha vita ya Badri, wakasema kwamba washirikina waliwachukuwa na kuwauliza, je mnataka kwenda kwa Muhammadi ili mshiriki nae vita?, wakajibu; hapana, sisi tunaenda Madina. Wakachua ahadi ya makubaliano kwamba waende Madina na wala wasishiriki vita na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake). Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akawambia: “ondokeni, tunatekeleza makubaliano yao, na tunamuomba Mwenyezi Mungu msaada”[8]. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) hakuwaamrisha washiriki nae vita kuwapiga makafiri kwa ajili ya kutekeleza ahadi


7.Msaliti asifurahi kwa kufaulu, wala matarajio anayo yatarajia kwa usaliti wake, atambue kwamba mwisho wake ni fedheha kubwa.

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amesema:

“kila msaliti anabendera, itasimikwa kwa ajili ya usaliti wake siku ya Kiyama”[9].

Hata kama Msaliti akijua namna ya kupangilia na kuratibu mambo yake, ili asifedheheshwe mbele ya watu, je ataenda wapi siku ya Kiyama na bendera imesimikwa kuonyesha usaliti wake mbele ya viumbe wote?!


8.Usijitafutie sababu ya kufanya hiyana, au uongo , au usaliti, au kuvuka mipaka katika ugomvi, hata kumfanyia aliye kufanyia, tambua kwamba mwislam anafuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala si matamanio yake.

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amesema:

“Tekeleza amana kwa aliye kuamini, na wala usimfanyie hiyana aliye kufanyia hiyana”[10].

9.Amesema mshairi

Achana na tabia za watu wasio kuwa na tabia njema***shikamana na tabia za watu bora na wenye adabu

Ukiombwa ufanye usaliti au ukiamrishwa***kimbia ujiokoe kukimbia kwa milele.


10.Akasema mwingine:

Ukweli anauzoea mkarimu mwenye matarajio ya  kukutana na Mwenyezi Mungu*** na uongo anauzoe dhalili aliye feli. Achana na muongo, na usimfanye kuwa rafiki yako***hakika muongo ni rafiki mbaya.


Marejeo

  1. Ufafanuzi wa Al-Nawawi juu ya Muslim (2/47)
  2. .""Fasihi ya Kinabii"" cha Muhammad Abdul Aziz al-Khouli (uk. 18)
  3. .Al-Bukhari (6094), na Muslim (2607), kutoka kwa Ibn Masoud
  4. .Al-Bukhari (6096), kutoka kwa Samra bin Jundab
  5. .Al-Bukhari (2680), na Muslim (1713), kutoka kwa Ummu Salamah, Mungu amuwiye radhi
  6. .Al-Bukhari (33), na Muslim (59), kutoka kwa Abu Hurairah
  7. .Al-Bukhari akielezea, Kitabu cha Imani, Sura: Hofu ya Muumini juu ya matendo yake kubatilika bila kujua
  8. .Muslim (1787)
  9. .Al-Bukhari (3188) na Muslim (1735)
  10. .Abu Daawuud (3534).



Miradi ya Hadithi