عن عبدِ الله بنِ عُمرَ رضي الله عنهما: أنه طلَّقَ امرأتَه وهي حَائضٌ على عِهدِ رسولِ الله ﷺ تطليقةً واحدةً، فسأل عمرُ بن الخطاب رضي الله عنه رسولَ الله ﷺ عن ذلك، فتغيَّظ رسولُ الله ﷺ، ثم قال رسولُ اللهِ ﷺ: «مُرْهُ فليراجعها، ثم ليُمسِكْها حتى تطهر، ثم تحيض، ثم تطهر، ثم إن شاء أمسك بعدُ، وإن شاء طلَّق قبل أن يمسَّ، فتلك العدةُ التي أَمَر اللهُ أن تطلَّق لها النساءُ»؛ متفقٌ عليه وفي لفظ لمسلم: ((مُرْه فليراجِعها، ثم ليطلقها طاهرًا أو حاملًا))


Kutoka kwa Abdullah bin Omar, Mwenyezi Mungu awawie radhi:

1. Alimtaliki mkewe akiwa katika hedhi, Kwenye wakati wa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kwa talaka moja, 2. Omar Ibn Al-Khattab akamuuliza Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam kuhusu hilo, 3. Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, akakasirika. 4. kisha Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam akasema: “Mwambie amrudishe, kisha abakie nae mpaka atoharike, kisha apate hedhi, kisha atoharike, 5. kisha akitaka ataishi naye baada ya hapo, na akipenda atamwacha kabla ya kumgusa (kumwingia). 6. huo ndio utaratibu ambao Mwenyezi Mungu ameamrisha kuachwa kwao wanawake.” Wameafikiana bukhari na muslim. Imepokewa, katika riwaya ya Muslim: Ibn Umar amesema: alisoma Mtume Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam aya hii : “Ewe Mtume, ikiwa utawataliki wanawake, basi wataliki kabla ya ada yao" . 7. Na katika mapokezi ya Imamu Muslim (kwamba Mtume alisema) " Muamrishe amrudishe, kisha ampe talaka akiwa msafi au mjamzito"

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao.”

[Talaka: 1]

Na Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Na wenye mimba eda yao ni mpaka watakapo zaa” .

[Talaka: 4]

Miradi ya Hadithi