عن ابن عبَّاسٍ رضي الله عنهما قال: كنتُ خَلْفَ رسولِ الله ﷺ يومًا، فقال: «يا غلامُ، إنِّي أُعلِّمُكَ كلماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ،احفَظِ اللهَ تَجِدْه تُجاهَكَ،إذا سألْتَ فاسأَلِ اللهَ، وإذا استَعَنْتَ فاستَعِنْ باللهِ، واعلَمْ أنَّ الأُمَّةَ لوِ اجتَمَعَتْ على أنْ يَنفَعوكَ بشيءٍ، لم يَنفَعوكَ إلَّا بشيءٍ قد كتَبَه اللهُ لكَ، ولوِ اجْتَمَعوا على أنْ يَضُرُّوكَ بشيءٍ، لم يَضُرُّوكَ إلَّا بشيءٍ قد كتَبَه اللهُ عليكَ، رُفِعَتِ الأقلامُ وجَفَّتِ الصُّحُفُ»

Kutoka kwa Ibn wa Abbaas (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yake), amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema:

1. “Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno (haya): 2. Mhifadhi Mwenyezi Mungu 3. Ili naye akuhifadhi 4. Muhifadhi Mwenyezi Mungu utampata mbele yako (kwa kila jambo lako) 5. Pindi utakapo omba, muombe Mwenyezi Mungu 6. Na ukitaka msaada basi taka msaada  kwa Mwenyezi Mungu 7. Tambua kwamba jamii ikikubaliana kukusaidia kwa lolote, haiwezi kukusaidia ila jambo ambalo Mwenyezi Mungu amekuandikia, na lau ikikubaliana ikudhuru kwa lolote, haiwezi kukudhuru ila kwa jambo ambalo Mwenyezi Mungu amekuandikia. 8. Kalamu imesha nyanyuliwa na karatasi zimesha kauka.  

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu

 " Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada. suratul Faatiha aya ya 5

[Al-Fatihah: 5]

Amesema Mwenyezi Mungu:

" Na timizeni ahadi yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na niogopeni Mimi tu."

[Al-Baqarah: 40]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Na Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea ila Yeye. Na akikutakia kheri, basi hapana awezaye kurudisha fadhila yake ". .

[Yunus: 107]

Amesema Mwenyezi Mungu:

"Hayo hivyo ni kwa ajili tumuepushe na uovu na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walio safishwa "

 [Yusuf: 24]

Amesema Mwenyezi Mungu:

 "Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni".

[Ghafir: 60]

 

Amesema Mwenyezi Mungu: " Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi". 

[Al-Hadid: 22]

Miradi ya Hadithi