عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: رأيتُ النبيَّ ﷺ يَرْمي على راحلتِهِ يومَ النَّحْرِ، ويقول: «لِتأخُذوا مناسكَكم؛ فإني لا أدْري لعلِّي لا أحُجُّ بعد حَجَّتي هذه.
عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: رأيتُ النبيَّ ﷺ يَرْمي على راحلتِهِ يومَ النَّحْرِ، ويقول: «لِتأخُذوا مناسكَكم؛ فإني لا أدْري لعلِّي لا أحُجُّ بعد حَجَّتي هذه.
Kutoka Kwa Jaber radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie amesema: Nilimuona Mtume Rehema na Amani zimshukie, akitupa mawe akiwa juu ya kipandwa Siku ya kuchinja. Huku Akisema: “Ili mpate kujifunza taratibu zenu; Sijui huenda sitahiji baada ya Hija hii.”
Amesema Mwenyezi Mtukufu:
“Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia sio dhambi juu yake, kwa mwenye kumcha Mwenyezi MUngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake”
[Al-Baqarah: 203].
Na akasema aliye tukuka zaidi:
“Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao” .
[An-Nisa: 80]
Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:
“Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao”.
[An-Nahl: 44]
Pia amesema Allah mwenye nguvu:
“Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu”.
[Al-Hashr: 7]