عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: رأيتُ النبيَّ ﷺ يَرْمي على راحلتِهِ يومَ النَّحْرِ، ويقول: «لِتأخُذوا مناسكَكم؛ فإني لا أدْري لعلِّي لا أحُجُّ بعد حَجَّتي هذه.

Kutoka Kwa Jaber radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie amesema: Nilimuona Mtume Rehema na Amani zimshukie, akitupa mawe akiwa juu ya kipandwa Siku ya kuchinja. Huku Akisema: “Ili mpate kujifunza taratibu zenu; Sijui huenda sitahiji baada ya Hija hii.” 

Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi waalihi wasallam alitupa mawe Jamarat al-Aqabah siku ya kafara akiwa amempanda ngamia wake, na akawaamrisha maswahaba zake kuchukua taratibu za Hijja,huenda hatohiji baada ya Hijja hiyo, na ndivyo ilivyokuwa.

Miradi ya Hadithi