عن أنس رضي الله عنه قال: قَدِمَ رسولُ الله ﷺ المدينةَ ولهم يومانِ يَلعبون فيهما، فقال: «ما هذانِ اليومانِ؟!» قالوا: كنا نلعَب فيهما في الجاهلية، فقال رسول الله ﷺ: «إن الله قد أبدلَكم بهما خيرًا منهما؛ يومَ الأضحى، ويومَ الفِطر»
عن أنس رضي الله عنه قال: قَدِمَ رسولُ الله ﷺ المدينةَ ولهم يومانِ يَلعبون فيهما، فقال: «ما هذانِ اليومانِ؟!» قالوا: كنا نلعَب فيهما في الجاهلية، فقال رسول الله ﷺ: «إن الله قد أبدلَكم بهما خيرًا منهما؛ يومَ الأضحى، ويومَ الفِطر»
Kutoka kwa Anas amesema:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie alikuja Madina na watu wa madina walikuwa na siku mbili za kucheza sikukuu, akasema Mtume: “Siku mbili hizi ni zipi?” Wakasema: Tulikuwa tukisherekea kabla ya Uislamu, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani ziwe juu yake akasema: “Mwenyezi Mungu amewabadilishia kwa kilicho bora kuliko hizo siku mbili; Siku ya al-Adh-haa na siku ya al-Fitwr.”
Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:
“Na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru”
[Al-Baqarah: 185].
Amesema Mwenyezi Mungu:
“Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake”
[Al-Baqarah: 203].
Akasema Mtukufu:
“Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri”
[An-Nisa: 2].
Pia akasema aliyetukuka:
“Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya”
[Yunus: 58]