عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ قَالَ:  «مَثَلُ القَائِمِ عَلَى حُدُودِ اللَّه وَالوَاقِعِ فِيهَا، كَمَثَلِ قَوْمٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ؛ فَأَصَابَ بَعْضُهُمْ أَعْلاهَا، وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا، فَكَانَ الَّذِينَ في أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوْا مِنَ المَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقَهُمْ، فَقَالُوا: لَو أَنَّا خَرَقْنَا في نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤْذِ مَنْ فَوْقَنَا، فَإِنْ يَتْرُكُوهُمْ وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعًا، وَإِنْ أَخَذُوا عَلى أَيْدِيهِمْ نَجَوْا، وَنَجَوْا جَمِيعًا»

Kutoka kwa Al-Nu’man bin Bashir Mwenyezi Mungu awe radhi naye, Kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, amesema:

“Mfano wa mwenye kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu na akashikamana nayo ni kama watu waliosongamana katika meli. Baadhi yao wakawa sehemu yake ya juu, na baadhi sehemu yake ya chini, ikawa waliokuwa chini, wanapochota maji, wanapita kwa wale walioko juu yao. Na wakasema: Afadhali tungelitoboa katika sehemu yetu, ili tusiwaudhi walioko juu, Wakiwaacha na kufanya wanavyotaka, wote wataangamia, na wakizuiliwa mikononi mwao wataokoka wote kwa ujumla” 


Muhtasari wa Maana

Ikiwa mipaka na kuamrisha mema na kukataza maovu itawekwa sawa, basi watu wote wataokoka, na kama sivyo watu wote wataangamia, Muasi ataangamizwa kwa kuasi kwake, na aliyenyamaza akaacha kukemea maovu na kuamrisha mema, ataangamizwa kwa hilo.

Miradi ya Hadithi