عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ قَالَ:  «مَثَلُ القَائِمِ عَلَى حُدُودِ اللَّه وَالوَاقِعِ فِيهَا، كَمَثَلِ قَوْمٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ؛ فَأَصَابَ بَعْضُهُمْ أَعْلاهَا، وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا، فَكَانَ الَّذِينَ في أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوْا مِنَ المَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقَهُمْ، فَقَالُوا: لَو أَنَّا خَرَقْنَا في نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤْذِ مَنْ فَوْقَنَا، فَإِنْ يَتْرُكُوهُمْ وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعًا، وَإِنْ أَخَذُوا عَلى أَيْدِيهِمْ نَجَوْا، وَنَجَوْا جَمِيعًا»

Kutoka kwa Al-Nu’man bin Bashir Mwenyezi Mungu awe radhi naye, Kutoka kwa Mtume, rehma na Amani zimshukie, amesema:

“Mfano wa mwenye kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu na akashikamana nayo ni kama watu waliosongamana katika meli. Baadhi yao wakawa sehemu yake ya juu, na baadhi sehemu yake ya chini, ikawa waliokuwa chini, wanapochota maji, wanapita kwa wale walioko juu yao. Na wakasema: Afadhali tungelitoboa katika sehemu yetu, ili tusiwaudhi walioko juu, Wakiwaacha na kufanya wanavyotaka, wote wataangamia, na wakizuiliwa mikononi mwao wataokoka wote kwa ujumla” 


Al-Nu’man bin Bashir bin Saad

Al-Nu’man bin Bashir bin Saad bin Tha’labah Al-Ansari, mwana wa mfalme, mwanachuoni, swahaba wa Mtume Rehma na Amani zimshukie na ni mtoto wa sahaba wake. Yeye ni miongoni mwa masahaba vijana kwa makubaliano ya wataalamu wa historia, na alikuwa mmoja wa viongozi wa Muawiyah, na alimteua kwenda mji wa Kuufa kwa muda, kisha gavana wa wilaya ya Damascus baada ya Fadala. Kisha mtawala wa Homsi ambao ni mji ulioko katikati mwa siria, hadithi zake zilitolewa na maimamu sita katika sunani zao, na hadithi zake ni chache, alikufa katika mwaka wa (64 AH) [1]

Marejeo

1. Rejea ufafanuzi wake katika: “Al-Tabaqat Al-Kubra” cha Ibn Saad (6/53), “Al-Isti’ab fi Ma’rifat Al-Ashab” cha Ibn Abd Al-Bar (4/1496), "'Usud Alghabati" cha Ibn Al-Atheer (4/550)

Miradi ya Hadithi