عن شَدَّادِ بْن أَوْسٍ: عَنِ النَّبِيِّ ﷺ: «سَيِّدُ الِاسْتِغْفَارِ أَنْ تَقُولَ: اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لاَ إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي؛ فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ " قَالَ: «وَمَنْ قَالَهَا مِنَ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا، فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ، فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، وَمَنْ قَالَهَا مِنَ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا، فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ، فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ».

Kutoka kwa Shaddad bin Aws Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka Kwa Mtume rehma na amani zimshukie, amesema:

1- “Bwana wa kuomba msamaha ni kusema: Ewe Mola Mlezi, wewe ni Mola wangu, hapana mungu ila Wewe, umeniumba na mimi ni mja wako. 

2- Na ninatimiza ahadi yako kwa kadri ya uwezo wangu. 

3- Najikinga Kwako kutokana na shari ya niliyoyafanya. 

4- Ninakiri neema yako juu yangu, na ninakiri dhambi yangu kwako. 

5- Basi nisamehe; kwani hakuna anayesamehe dhambi ila wewe." 

6- Akasema: “Na mwenye kusema hayo mchana akiwa na yakini nayo, basi akafariki mchana huo kabla ya kuingia jioni, bila shaka atakuwa ni katika watu wa Peponi” 

Shaddad bin Aws

Ni: Shaddad bin Aws bin Thabit bin Al-Mundhir Al-Ansari Mwenyezi Mungu awe radhi naye, Abu Yaala, mmoja wa masahaba mashuhuri na wanachuoni wao.Ubada bin Al-Samit Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: “Shaddad bin Aws alikuwa miongoni mwa waliopewa elimu na uvumilivu” Na Abu Darda’i, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu humpa mwanaadamu ilimu lakini hampi subira, na subira anampa lakini hampi ilimu. Na Abu Ya’laa Shaddad bin Aws alikuwa miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa elimu na uvumilivu.” Aliishi katika mji wa Hims huko Sham, na Umar ibn al-Khattaab, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alimteua kuwa mtawala wake, na alipouawa Othman bin Affan, Mwenyezi Mungu amridhie, alistaafu utawala wake. Alikuwa mwingi wa ibada, uchamungu, na khofu ya Mwenyezi Mungu. Alikufa huko Palestina katika mwaka wa hamsini na nane wa Hijrah, akiwa na umri wa miaka sabini na mitano  .[1]

Marejeo

  1. Rejea ufafanuzi wake katika: “Ma’rifat al-Sahaba” cha Abi Na’im (3/1459), “Al-Istiba’ fi Ma’rifat al-Ashab” cha Ibn Abd al-Barr (2/694), “Asad al-Ghaba” cha Ibn al-Atheer (2/613), “Al-Isaba fi Tamayoz al-Sahaba” cha Ibn hajar (3/258).


Miradi ya Hadithi