عَنْ أَبِي مُوسَـى الأشعريِّ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ، قَالَ: «مَثَلُ الْبَيْتِ الَّذِي يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ، وَالْبَيْتِ الَّذِي لَا يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ، مَثَلُ الْـحَيِّ وَالْـمَيِّتِ». 

وَلِلْبُخَارِيِّ: «مَثَلُ الَّذِي يَذْكُرُ رَبَّهُ، وَالَّذِي لَا يَذْكُرُ رَبَّهُ، مَثَلُ الحَيِّ وَالـمَيِّتِ».

Kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ariy, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema:

1- “Nyumba ambayo anatajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na nyumba asiyotajwa Mwenyezi Mungu ni kama walio hai na wafu. Na katika sahihi al-Bukhari: 

2- “Mfano wa mwenye kumtaja Mola wake Mlezi na yule asiyemtaja Mola wake Mlezi ni kama aliye hai na maiti.” 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:

“Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya”

[Al-An'am: 122]

Na allah aliyetakasika akasema:

“Na mkumbuke Mola Mlezi wako nafsini kwako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni. Wala usiwe miongoni mwa walio ghafilika” .

[Al-A’raf: 205]

Amesema Allah Mtukufu:

“Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutulia”.

[Ar-Ra'd: 28]

Amesema tena:

“Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru (41) Na mtakaseni asubuhi na jioni”.

[Al-Ahzab: 41, 42]

Miradi ya Hadithi