عَنْ أَبِي مُوسَـى الأشعريِّ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ، قَالَ: «مَثَلُ الْبَيْتِ الَّذِي يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ، وَالْبَيْتِ الَّذِي لَا يُذْكَرُ اللهُ فِيهِ، مَثَلُ الْـحَيِّ وَالْـمَيِّتِ». 

وَلِلْبُخَارِيِّ: «مَثَلُ الَّذِي يَذْكُرُ رَبَّهُ، وَالَّذِي لَا يَذْكُرُ رَبَّهُ، مَثَلُ الحَيِّ وَالـمَيِّتِ».

Kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ariy, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema:

1- “Nyumba ambayo anatajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na nyumba asiyotajwa Mwenyezi Mungu ni kama walio hai na wafu. Na katika sahihi al-Bukhari: 

2- “Mfano wa mwenye kumtaja Mola wake Mlezi na yule asiyemtaja Mola wake Mlezi ni kama aliye hai na maiti.” 

Abuu Muusaa Abdullahi Ibn Qays

Ni Abuu Muusaa Abdullahi Ibn Qays Ibn Sulaym Ibn Hudhdhwaari Ibn Harbi Ibn A’mir Ibn Ash-Ar Al-Ash-Ariy, kiongozi mkubwa, mwana fiqhi,(msomi wa sheria ya dini),swahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, mwenye kuhama mara mbili: ku-hamia habeshi na kuhamia madina(mji wa Mtume) alikua kiongozi katika mji wa basra katika ukhalifa wa Umaru Ibn Al-Khatwab (R. A) akawafundisha watu wa basra na akawapatia utambuzi juu ya dini yao, na akawasomesha qur’ani tukufu (kitabu cha Allah) na alikua ni bora sana katika maswahaba wa Mtume (s.a.w) kwa sauti ya kuiso-ma qur’ani tukufu.Alikufa mwaka (50:h)(1).

Marejeo

  1. 1 Rejea tafsiri yake katika: “Maarifaat al-Sahaba cha Abu Naim” (4/ 1749), “Kuna-sibishwa katika kuwajua Maswahaba kwa Ibn Abd al-Bar” (4/ 1762), “Asad al-Ghaba cha Ibn al. -Atheer” (5/306).


Miradi ya Hadithi