عن أبي هُرَيرة رضي الله عنه، أن رسول الله ﷺ قال: «قال اللهُ عزَّ وجلَّ: كلُّ عمَلِ ابن آدمَ له، إلَّا الصيامَ؛ فإنه لي، وأنا أَجْزِي به، والصِّيامُ جُنَّةٌ، وإذا كان يومُ صومِ أحدكم، فلا يَرْفُثْ، ولا يَصْخَبْ، فإن سابَّهُ أحدٌ أو قاتَلَهُ، فليقُلْ: إني امرؤٌ صائمٌ، والذي نفْسُ محمدٍ بيده، لَخُلُوفُ فمِ الصائم أطيبُ عند الله مِن ريحِ المِسْك، للصائمِ فَرْحتانِ يَفرَحُهما: إذا أفطَرَ فَرِحَ، وإذا لَقِيَ ربَّهُ فَرِحَ بصومِه»

Kutoka kwa Abu Hurairah, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimshukie amesema:

Amesema Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka: “Kila kitendo cha mwana wa Adamu ni chake isipokuwa kufunga. Funga ni yangu na nitailipa, Kufunga ni ngao. Na ikiwa ni siku ambayo mmoja wenu amefunga, basi asifanye uchafu au kupiga kelele, na mtu akimtukana au akimpiga, basi na aseme: Mimi ni nimefunga. Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, harufu inayotokatoka kinywani mwa mfungaji ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya miski. Mfungaji ana furaha mbili: anapofuturu hufurahi, na atapokutana na Mola wake Mlezi hufurahia saumu yake.”

Muhtasari wa Maana

Mtume Rehma Na Amani Zimshukie anaeleza baadhi ya fadhila za funga, ikiwa ni pamoja na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amemhifadhia ujira yeye mwenyewe bila ya yeyote kujua malipo yake, na kwamba funga inamzuia asiingie katika uasi na madhambi, na kwamba harufu ya kinywa cha mfungaji inapendeza kwa Mwenyezi Mungu, hata kama watu wanaichukia, na kwamba mfungaji atafurahi Siku ya Kiyama atapoona malipo ya funga yake, kama anavyofurahi duniani kwa Mwenyezi Mungu kumwafikisha kufunga.

Miradi ya Hadithi