عن أبي الدَّرْداءِ قال: سمعتُ رسولَ الله ﷺ يقولُ: «مَن سلَكَ طريقًا يَلتمِسُ فيه عِلمًا، سهَّلَ اللهُ له طريقًا إلى الجنةِ، وإنَّ الملائكةَ لَتضَعُ أجنحتَها رضًا لطالب العلم، وإنَّ طالبَ العلم يَستغفِرُ له مَن في السماء والأرض، حتى الحيتانُ في الماء، وإنَّ فضلَ العالِم على العابد كفضل القمرِ على سائر الكواكب، وإنَّ العلماءَ ورَثةُ الأنبياء، وإنَّ الأنبياءَ لم يورِّثوا دينارًا ولا درهمًا؛ إنما ورَّثوا العلمَ، فمَن أخذه أخَذ بحظٍّ وافرٍ».

Kutoka kwa Abuu Dar-Dai (r.a) amesema: nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake akisema:

1. “Mwenye kupita njia akitafuta elimu katika njia hiyo, Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi zaidi njia ya kwenda peponi. 

2. Na hakika malaika naapa kwa Allah wanaweka mbawa zao kumridhia mtafuta elimu,  

3. Na hakika mwenye kutafuta elimu wanamuombea msamaha viumbe wa mbinguni na ardhini, hata pia samaki katika maji. 

4. Na hakika ubora wa mwanazuoni kwa waja wa Mwenyezi Mungu ni kama ubora wa mwezi juu ya nyota zote. 

5. Na hakika wanazuoni ndio warithi wa mitume wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na hakika mitume wa Allah hawakurithiwa dinari wala dir-ham; bali si vinginevyo walirithiwa elimu, basi atakeichukuwa atakua amechukua fungu kubwa sana. 

Miradi ya Hadithi