عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «يَا أَبَا الْمُنْذِرِ، أَتَدْرِي أَيُّ آيَةٍ مِنْ كِتَابِ اللهِ مَعَكَ أَعْظَمُ؟» قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: «يَا أَبَا الْمُنْذِرِ، أَتَدْرِي أَيُّ آيَةٍ مِنْ كِتَابِ اللهِ مَعَكَ أَعْظَمُ؟» قُلْتُ: اللهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﱠ. فَضَرَبَ فِي صَدْرِي، وَقَالَ: «وَاللهِ لِيَهْنِكَ الْعِلْمُ أَبَا الْمُنْذِرِ».

Kutoka kwa Ubay bin Ka’b radhi za mwenyzi mungu ziwe juu yake amesema:

1- Alisema Mtume (Rehme na Amani zimfikie) :“Ewe Baba  Mundhir, je, unajua ni Aya gani katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 

2- Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi. 

3- Akasema: “ewe Baba Mundhir, unajua ni aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 

4- Nikasema: (Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa yeye, Aliye Hai, msimamizi wa kila jambo) (na hii ni aya ya 225 sura ya pili yaan ayutul kursiyu). 

5-(Mtume) Alipiga kifua changu, 

6- Na akasema: “Wallahi elimu itulizane kwako, ewe Baba Mundhir.” 

Muhtasari wa Maana

Hadith inaashiria kwamba Ayat al-Kursi ni aya kubwa na tukufu zaidi katika Qur’ani.

Miradi ya Hadithi