عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «يَا أَبَا الْمُنْذِرِ، أَتَدْرِي أَيُّ آيَةٍ مِنْ كِتَابِ اللهِ مَعَكَ أَعْظَمُ؟» قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: «يَا أَبَا الْمُنْذِرِ، أَتَدْرِي أَيُّ آيَةٍ مِنْ كِتَابِ اللهِ مَعَكَ أَعْظَمُ؟» قُلْتُ: اللهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﱠ. فَضَرَبَ فِي صَدْرِي، وَقَالَ: «وَاللهِ لِيَهْنِكَ الْعِلْمُ أَبَا الْمُنْذِرِ».

Kutoka kwa Ubay bin Ka’b radhi za mwenyzi mungu ziwe juu yake amesema:

1- Alisema Mtume (Rehme na Amani zimfikie) :“Ewe Baba  Mundhir, je, unajua ni Aya gani katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 

2- Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi. 

3- Akasema: “ewe Baba Mundhir, unajua ni aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 

4- Nikasema: (Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa yeye, Aliye Hai, msimamizi wa kila jambo) (na hii ni aya ya 225 sura ya pili yaan ayutul kursiyu). 

5-(Mtume) Alipiga kifua changu, 

6- Na akasema: “Wallahi elimu itulizane kwako, ewe Baba Mundhir.” 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu: 

Mwenyezi Mungu - hapana Mola ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu..

[Al-Baqarah: 255]

Amesema Mwenyezi Mungu: 

Ishara yoyote tunayo ifuta au tunayo isahaulisha tunailetea iliyo bora kuliko hiyo, au iliyo mfano wake. .

[Al-Baqarah: 106]

Amesema Mwenyezi Mungu: 

Bali hii (Qur'ani) ni Ishara zilizo wazi katika vifua vya walio pewa ilimu. Na hawazikatai Ishara zetu isipo kuwa wenye kudhulumu..

[Al-Ankabut:49]

Miradi ya Hadithi