عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «يَا أَبَا الْمُنْذِرِ، أَتَدْرِي أَيُّ آيَةٍ مِنْ كِتَابِ اللهِ مَعَكَ أَعْظَمُ؟» قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: «يَا أَبَا الْمُنْذِرِ، أَتَدْرِي أَيُّ آيَةٍ مِنْ كِتَابِ اللهِ مَعَكَ أَعْظَمُ؟» قُلْتُ: اللهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﱠ. فَضَرَبَ فِي صَدْرِي، وَقَالَ: «وَاللهِ لِيَهْنِكَ الْعِلْمُ أَبَا الْمُنْذِرِ».

Kutoka kwa Ubay bin Ka’b radhi za mwenyzi mungu ziwe juu yake amesema:

1- Alisema Mtume (Rehme na Amani zimfikie) :“Ewe Baba  Mundhir, je, unajua ni Aya gani katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 

2- Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi. 

3- Akasema: “ewe Baba Mundhir, unajua ni aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyo kubwa kwako?” 

4- Nikasema: (Mwenyezi Mungu, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa yeye, Aliye Hai, msimamizi wa kila jambo) (na hii ni aya ya 225 sura ya pili yaan ayutul kursiyu). 

5-(Mtume) Alipiga kifua changu, 

6- Na akasema: “Wallahi elimu itulizane kwako, ewe Baba Mundhir.” 

Ubay bin Kaab bin Qais, Abu Al-Mund-hir Al-Madani

Jina lake ni: Ubay bin Kaab bin Qais, Abu Al-Mund-hir Al-Madani, bwana wa wasomaji, na mmoja kati ya maswahaba watukufu, na alikuwa mmoja wa maswahaba ulioshiriki kiapo cha utii kwa Mtume chini ya mti cha mara ya pili, na alishiriki katika vita vya Badr na vita nyinginezo. na alikuwa wa kwan-za kumwandikia Mtume (rehme na Amani zimfikie), alifariki katika ukhalifa wa Uthman mwaka wa 30(1)1 

Marejeo

  1. Tazama ufafanuzi wake katika: Al-Isti'ab fi Ma'rifat Al-Sahaba cha Ibn Abd Al-Bar (1/65), Asad Al-Ghaba cha Ibn Al-Atheer (1/168), na Al-Isbah fi Tamaiz. Al-Sahaba cha Ibn Hajar (1/180).


Miradi ya Hadithi