عَنْ مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ «إنَّ أخْوَفَ ما أخافُ عليكم الشِّركُ الأصْغَرُ»، قالوا: وما الشِّركُ الأصْغَرُ يا رسولَ اللهِ؟ قال: «الرِّياءُ؛ يقولُ اللهُ - عزَّ وجلَّ - لهم يومَ القِيامةِ إذا جُزِيَ الناسُ بأعمالِهم: اذْهَبوا إلى الذين كنتُم تُراؤون في الدُّنيا، فانظُروا هل تَجِدون عِندَهُم جزاءً؟!»

Kutoka kwa Mahmood bin Labiid amesema:

amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake): 1. “Hakika ninalo ogopea kwenu zaidi ni shirki ndogo” 2. Wakasema: shirki ndogo ni nini eh Mtume wa Mwenyezi Mungu? 3. Akasema: ni riya yaani kufanya kwa kujionesha 4. Mwenyezi Mungu Mtukufu atawambia siku ya kiyama baada ya watu kulipwa kwa matendo yao: 5. “Nendeni kwa mlio kuwa mnajionesha kwao, muone je watakulipeni?!”


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu:

“Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni udhalimu ulio mkubwa” .

[Luqman: 13]

Pia Amesema Mwenyezi Mungu:

“Hakika wanaafiki wanamhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwahadaa wao. Na wanapo sali husali hali wakiwa wavivu, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo sana” .

[An-Nisaa: 142]

Na Mwenyezi Mungu amesema:

“Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama afanyavyo mtu anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho.”

[Al-Baqarah: 264].

Na Mwenyezi Mungu amesema:

“Na hakika yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu matendo yako yataharibika, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kupata hasara” .

[Al-Zumar: 65]

Pia Amesema Mwenyezi Mungu:

“Wanao taka maisha ya dunia na pumbao lake tutawalipa humo vitendo vyao kaamili. Na wao humo hawatopunjwa (15) Hao ndio ambao hawatakuwa na kitu Akhera ila Moto, na yataharibika waliyo yafanya, na yatapotea bure waliyo kuwa wakiyatenda”

[Hud: 15, 16]

Amesema Mwenyezi Mungu:

“Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, na wawe waongofu,” .

[Al-Bayinat: 5]

Miradi ya Hadithi