عَنْ مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ «إنَّ أخْوَفَ ما أخافُ عليكم الشِّركُ الأصْغَرُ»، قالوا: وما الشِّركُ الأصْغَرُ يا رسولَ اللهِ؟ قال: «الرِّياءُ؛ يقولُ اللهُ - عزَّ وجلَّ - لهم يومَ القِيامةِ إذا جُزِيَ الناسُ بأعمالِهم: اذْهَبوا إلى الذين كنتُم تُراؤون في الدُّنيا، فانظُروا هل تَجِدون عِندَهُم جزاءً؟!»

Kutoka kwa Mahmood bin Labiid amesema:

amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake): 1. “Hakika ninalo ogopea kwenu zaidi ni shirki ndogo” 2. Wakasema: shirki ndogo ni nini eh Mtume wa Mwenyezi Mungu? 3. Akasema: ni riya yaani kufanya kwa kujionesha 4. Mwenyezi Mungu Mtukufu atawambia siku ya kiyama baada ya watu kulipwa kwa matendo yao: 5. “Nendeni kwa mlio kuwa mnajionesha kwao, muone je watakulipeni?!”


Mahamood bun Labiid Mahamood bun Labiid bun u’qba

Nuaim, Mahamood bun Labiid bun u’qba al-answaari(ni katika waislaam walio mpokea Mtume Madina) kabila la Aus, ukoo wa Ash-hari al-madan. Amezaliwa Madina kipindi Mtume bado yuko hai, na hakuhifadhi hadithi nyingi kutoka kwake kwa sababu ya udogo wa umri, alikuwa anapokea Hadith kutoka kwa Umar, Uthman na Raafi’I bun Khadiij. Baba yake dio sababu ya kuteremka aya ya kumruhusu asifunge ambaye hajiwezi. Amefariki katika mji wa Madina mwaka (97H)  [1]

Marejeo

1. Rejea  yake ufafanuzi wake katika: “Maarifaat al-Sahaba” na Abu Nu’aym (4/1846), “aliastieab fi maerifat al'ashabi"na Ibn Abd al-Bar (4/1770), “Asad al-Ghaba” na Ibn al-Atheer (3/357), “Al-Isbah fi Tamazu al-Sahaba” cha Ibn Hajari Asqalani (4/267) .


Miradi ya Hadithi