عن أبي يحيى صهيب بن سنان قال: قال رسول الله ﷺ: «عَجَبًا لأَمْرِ المُؤْمِنِ، إنَّ أمْرَهُ كُلَّهُ خَيْرٌ، وليسَ ذاكَ لأَحَدٍ إلَّا لِلْمُؤْمِنِ، إنْ أصابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ، فَكانَ خَيْرًا له، وإنْ أصابَتْهُ ضَرَّاءُ، صَبَرَ فَكانَ خَيْرًا له».

Kutoka kwa Abu Yahya Suhaib bin Sinan, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie.

1- “Ni la kustaajabisha jambo la Muumini, kwani mambo yake yote ni kheri, na hayo si ya kila mtu isipokuwa kwa Muumini peke yake. 

 2- Ikimpata kheri hushukuru, na inakuwa ni kheri kwake. 

3- Na yakimpata matatizo husubiri, na inakuwa ni kheri kwake.” .


1- Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anastaajabu juu ya Muumini na hali yake mbele ya Mwenyezi Mungu, Utukufu ni Wake, nao ni mshangao wa ridhaa na furaha, kwa kuwa muumini katika hali zake zote analipwa.

2- Iwapo Mwenyezi Mungu angemjaalia baraka iliyomfurahisha nafsi yake, mali yake, au familia yake, basi anaipokea baraka hiyo kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili yake. Ambapo Mwenyezi Mungu humzidishia neema yake, na humlipa shukrani zake.
3- Na akifikwa na yale yanayomdhuru na yanamuumiza, basi huvumilia mateso, na kuridhika nayo, na anataraji malipo kwa Mwenyezi Mungu.
Hadithi hii inajumuisha hukumu zote za Mwenyezi Mungu kwa waja Wake. Ama atawajaribu kwa shari au kwa kheri, na Akasema, Allah Mtukufu:

“Na tutakujaribuni kwa shari na kheri kama mtihani”

[Al-Anbiya: 35]

; Muumini akivumilia shari na kushukuru mema, basi ameitimiza imani yake, na ndio maana waliotangulia wakasema: Imani ni nusu mbili; Subira ni nusu na nusu ni kushukuru, kama alivyo sema Allah mwenye kutukuka:

“Hakika katika hayo zimo Ishara kwa kila mwenye subira na mwenye kushukuru”[1]  .

[Ibrahim: 5]


1- (1) Muumini wa kweli ambaye ameridhika na matakwa ya Mwenyezi Mungu na hatima yake, ambaye ni mvumilivu kwa yale yanayomfika, na ambaye anashukuru neema za Mwenyezi Mungu juu yake - mambo yake yote yanaendeshwa kwa apendavyo. Kwa hivyo hakikisha kufikia kiwango cha kuridhika na kushukuru, hadhi yako itakuzwa na matendo yako mema yataongezeka.


2- (2) Shukuru neema za Mwenyezi Mungu juu yako ambazo hazihesabiki, ni baraka ngapi ziko katika dini yako, maisha yako, roho yako, afya yako, elimu yako, biashara yako, kazi yako, pesa yako na familia yako, ambazo mmo ndani yake mmeghafilika nazo  na hamkuwatimizia haki yake ya kushukuru na kuzitambua!


3- (2) Shukrani inapelekea kuongezeka na baraka. Basi kuwa na shukurani ili uongezewe zaidi.


4- (3) Pambana na majaribu kwa moyo wa Muumini ambaye anajua kwamba yaliyompata hayakuwa yamkose, na kwamba Qadari ya Mungu ni lazima itimie .


5- (3) Usipapatike unapo fikwa na Qadari ya Mwenyezi Mungu, kwani balaa ni lenye kukufika tu bila shaka, sasa mwenye subra ziko zote hupata malipo na akawa mwenye msaada, na mwenye kukata tamaa anaambulia thambi na kudhalilika.


6- (3) Saiyd bin Jubair-Mwenyezi Mungu amrehemu- amesema: “Subira ni kukiri kwa mja kwa Mwenyezi Mungu kwamba yaliyompata hutoka kwake, hutaraji malipo yake kwa Mwenyezi Mungu na matumaini ya malipo yake. Na mtu anaweza kuingiwa na khofu wakati anapiga kelele, na hakuna kinachoonekana kwake isipokuwa subira” [2].


7- (3) Ibn Rajab-Mwenyezi Mungu amrehemu- amesema: “Watu wenye kuridhika wakati fulani wanaiona hekima ya Allah Mwenye kuwajaribu waja wake na wema wake kwa mja wake katika dhiki, na kwamba hashutumiwi katika maamzi yake. wakati mwingine wanaona malipo ya kuridhika na hukumu, hivyo husahau maumivu ya kile kilicho kadiriwa kwao, na wakati mwingine wanaona ukubwa, utukufu na ukamilifu wa mwenye kuwatahini, hivyo wanajikita Katika kushuhudia hayo mpaka inawasahaulisha maumivu, na hali hii wanaifikia watu maalumu wenye elimu na mapenzi, mpaka wakti mwengine wanona ladha kwa yanayo wasibu kwa sababu wanazingatia kuwa yanatoka kwa kipenzi chao, kama walivyosema baadhi yao: Amewatilia ladha katika adhabu yake. [3]” .


8- Baadhi ya wafuasi baada ya maswahaba waliulizwa kuhusu hali yake wakati wa ugonjwa wake, na akasema: “Hali hii inapendeza kwake na inapendeza kwangu”[4] .


9- Omar Ibn Al-Khattab, radhi za Allah na amani ziwe juu yake, amesema: Lau kama subira na shukrani zingekuwa ngamia wawili, nisingejali ni yupi niliyempanda [5] .


10- Mshairi alisema:
Inasikitisha sana kwamba shukrani yangu haipo = kutokana na ninayoyatenda, na kwamba wema wako inazungumza
Na ninakiona kitendo kutoka kwako, kisha nakificha = basi mimi ni mwizi wa fadhila na ukarimu.


11- Wengine walisema:
Ikiwa mimi kushukuru neema za Allah ni baraka kwangu, = kwa ajili yake, ninapaswa kumshukuru
Basi shukrani itatokeaje isipokuwa kwa neema yake = hata kama siku ni ndefu na maisha ni yenye kuendelea
Akipata kheri furaha hushamiri = na akipata dhiki malipo hufuata.
Hakuna lolote isipokuwa ndanimwe kuna neema = udanganyifu, siri, na umma huipunguza.

Marejeo

  1. "Jami' al-Masa'il" cha Ibn Taymiyyah - kundi la kwanza (uk. 165).
  2. eidat alsaabirin wadhakhirat alshaakirina" cha Ibn Al-Qayyim (uk. 97).
  3.   “Jami’ al-‘Ulum wa’l-Hukam” cha Ibn Rajab (1/487). 
  4.   “Jami’ al-‘Ulum wa’l-Hukam” cha Ibn Rajab (1/487).
  5.    eidat alsaabirin wadhakhirat alshaakirina" cha Ibn Al-Qayyim (uk. 94).


Miradi ya Hadithi