عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّةِ. وَإِنَّمَا لِامْرِئٍ مَا نَوَى. فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِـهِ، فَهِجْرَتُهُ إِلَى اللهِ وَرَسُولِـهِ. وَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيَا يُصِيبُهَا، أَوِ امْرَأَةٍ يَتَزَوَّجُهَا، فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ» متفق عليه.

Kutoka kwa Umar bin Al-Khattab, (r.a) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.).

1. Hakika matendo huhesabika kwa nia tu. 

2. Na hakika kila mtu atalipwa kwa alilokusudia. 

3. Basi atakaekuwa kuhama kwake ni kwa ajili Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kuhama kwake ni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. 

4. Na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya dunia ili aipate, au mwanamke ili amuoe, basi kuhama kwake ni lile aliloliendea.” (Imepokelewa na Imam Bukhari na Muslimu).

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

﴾Sema: Mola Mlezi wangu ameamrisha uadilifu, na mumuelekezee nyuso zenu kila mnapo sujudu, na muombeni Yeye kwa kumsafia Dini. Kama alivyo kuumbeni mwanzo ndivyo mtavyo rudi, ﴿

(a`araaf :9)

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

﴾ Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu, na hata kama wangechukia makafiri. ﴿ 

(Ghaafir :14)

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

﴾Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.

(Shuuraa :20)

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

﴾Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. ﴿ .

(Nisaa :100 )

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu pia

﴾Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha. ﴿

Miradi ya Hadithi